Asante sana Boss Ruge kwani wewe ndiye uliyenipa nguvu na ushauri mkubwa katika Blogg hii.

Posted by Apolinary Macha on 10:55 with No comments


Moyo wangu umeumia sana baada ya kuona hutoweza kuona tena kazi za mikono yangu katika Blog yangu. Sitosahau siku uliyopitia My Blog tulipokwepo THT, uliiona kwenye CV yangu ukawa unaitazama na uliponiita uliniambia kuhusiana na hii Blogg na kuniuliza maswali mengi katika kufahamu uandishi wangu, nia yangu. Nakumbuka ulinisifia kwa uandishi na kuandika mambo ambayo yanawagusa raia wengi wa kawaida, ulinishauri nisiache na niendelee. Blog hii ndiyo iliyokufanya ukatamani sana kuonana na mimi, na tangu siku ile ulinipokea na nikawa kijana wako.

Tumefanya kazi kwa pamoja, umenilea na kunifundisha mengi sana katika kazi mbalimbali. Umenijali kama mdogo wako na ukanipa kazi ya kukusaidia uandishi wa Projects zako na uliniahidi ipo siku tutafanya kitu katika hii Blogg. Kwa bahati mbaya malengo yetu hayakuweza kwenda kama tulivyopanga. Nitaendelea kufanya uandishi wa Blogg hii na sitosimama.

Daima nitakuombea, na nina imani maisha yako baada ya haya ya duniani ni mazuri kutokana na mengi mema uliyoyafanya na ulitumia nafasi yako kutuinua vijana wengi.

Asante sana Boss Ruge kwa kila kitu na kwa nafasi ambayo umenipatia. Asante sana kwa kuniamini na ninatoa ahadi ya kuyatimiza yale niliyokuahidi. Utaishi milele kwenye mioyo yetu.

Asante sana.

#JasiriMuongozaNjia