Itafuteni KWELI, na KWELI Itawaweka Huru.
Posted by Apolinary Macha on 10:32 with 1 comment
Itafute Kweli na Kweli itakuweka Huru |
Watu wengi wamelala. Kulala ni nini?
Kulala ni kutofahamu uhalisia wa Maisha. Kutofahamu uhalisia wa maisha ni GIZA la ufahamu.
Ninaposema ni giza la ufahamu ina maana ya kwamba ni kizuizi cha ufahamu kuona vyema.
Ndio maana vitabu vya imani vimesema “Itafuteni KWELI, na KWELI itawaweka huru”.
Je KWELI ni nini?
KWELI ni uhalisia.
KWELI ni mwanga.
KWELI ni REALITY.
Wengi hawaijui KWELI, wengi wanafikiri wanaijua kweli lakini sio kweli.
Je KWELI utaipata wapi?
KWELI haipo kwenye imani, kwenye dini, kwenye sayansi, nyumbani, kanisani, msikitini wala haipo hekaluni.
KWELI ipo kila mahali.
Je kama ipo kila mahali ni kwanini itafutwe?
Kuitafuta KWELI sio kama kuitafuta kitu kilichopotea au kilichojificha, ni KUITAMBUA KWELI.
Ni ngumu sana kuitambua, ni ngumu kuitambua KWELI kuliko kutafuta kilichopotea.
Kilichopotea kimejificha lakini hakionekani lakini KWELI haijajificha lakini ni ngumu kuitambua na kuipata.
Je UTAIPATAJE KWELI?
Kwa kuitambua ndani mwako.
Unayo wakati wote, umezaliwa nayo na unaendelea kuishi nayo.
Ipo moyoni mwako na AKILINI mwako.
Itambue KWELI, na utakuwa huru.
Utakuwa huru na mateso ya dunia, shida, taabu, mawazo, fikra, machungu, hisia na mashikilio yote ya kidunia ni kimwili.
KWELI itakuweka huru.
KWELI itaungana na wewe daima.
KWELI NI MUNGU.
KWELI NI UHALISIA.
KWELI NI KUAMKA.
KWELI NI MWANGA.
Naitambuaje {KWELI} ndaniyangu
JibuFuta