Maisha ni Mafupi - Ishi katika Malengo Yako

Posted by Apolinary Macha on 14:36 with No comments

Maisha ni Mafupi; Sema unachotaka kusema, Tenda unachotaka kutenda; Usisubiri ufike muda ambao utajuta kutoishi sahihi kama ulivyotaka wewe -Lori Descheme


Muda hausimami, kila siku muda unaendelea kwenda mbele na nyakati zinazidi kubadilika. Katika maisha ya mwanadamu kuna wakati mwili na akili vinakuwa na nguvu ya kutosha katika kufurahia maisha na kuna wakati tunakosa nguvu ya mwili na akili. Hii ni hasa tukiwa uzeeni na mwili ukiwa umeshachoka.

Kuna muda tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunayatumia maisha yetu kiusahihi katika kuishi njia sahihi tunayotazamia. Isifike wakati ukajutia maamuzi ambayo uliyafanya, hivyo kuwa makini na maamuzi yote utendayo. Ili kila muda unavyozidi kwenda mbele, uwe umetimiza malengo yako mengi na kuishi katika maisha ambayo haujutii kuyachagua.

Maisha ni mafupi - Ishi katika malengo yako.