Mwisho wa Kanuni kuu 10 Za Akili na Ulimwengu. (Ujumbe)

Posted by Apolinary Macha on 17:48 with No comments
Mawazo ni uhalisia.
Mawazo ni uhalisia unaosubiri muda fulani na space kufika na uhalisia huo kuonekana katika ulimwengu wako. Kinachofanya uone mawazo sio uhalisia ni muda. Kama kungekuwa hakuna kipindi fulani cha wakati  baina ya kilichopo akilini mwako na uhalisia wako ungeona ni kitu kimoja, lakini kutokana na muda unaona ni viwili tofauti na unaweza ukabisha. Inahitaji umakini wa kijitambua, kujichunguza na kuwa mvumilivu muda ufikapo utaona uhalisia wake. Leo hii unaweza ukawa ulishasahau experience hii kama uliwahi kuiwaza, au labda uliwahi kuamini hivi, n.k na vyote hivi vinakujengea ulimwengu na experience hii ya sasa huku ukiwa umeshasahau kama experience hii ilikwepo katika ufahamu wako au kulikwepo na uhalisia huu lakini hukuweka umakini kutambua.

Kama unakumbuka kanuni ya kwanza "KILA TENDO LINA MATUNDA YAKE/ CAUSE AND EFFECT/KILA JAMBO LINA CHANZO CHAKE". Chanzo hakina tofauti na tokeo. Ukipanda maembe utavuna maembe kwani chanzo hakina tofauti na matokeo. Tofauti inaweza kuwepo kwenye hali au vitu lakini usawa ni lazima utakwepo. Hivyo kama chanzo hakina tofauti na matokeo, chanzo na matokeo ni kitu kimoja bali kinachofanya tuone ni tofauti ni wakati wa utimilifu wa tokeo baada ya chanzo kuwepo.

Dunia yako ya ndani haina tofauti na dunia yako ya nje. Lakini kutokana na wakati na space (time and space) inakuwa ni ngumu kuwaza kuangalia tokeo kulinganisha na chanzo.

MARUDIO
  1. Kila jambo, kitu au hali kina Chanzo.
  2. Wewe ndiye mfikiriaji wa pekee na hakuna anayeweza kutumia akili yako kufikiria na kufanya maamuzi kwa uwezo sawa ulio nao wewe katika kutumia akili yako.
  3. Chochote unachokiwekea umakini huchukua nafasi kubwa katika uhalisia wako.
  4. Kilichopo katika ulimwengu wako wa ndani hutengeneza uhalisia wako wa nje yako.
  5. Hakuna chochote cha kubadilisha nje yetu bali kubadilisha reality yetu huanza kwa kubadilisha ulimwengu wa ndani kwanza. 
  6. Kutokana unawaza kila wakati na mara nyingi kuna kinachoendelea akilini basi na kila wakati na kila jambo linapoendelea akilini huweka uhalisia fulani katika maisha yetu na mtazamo kwa ujumla.
  7. Huwezi kuwa na hisia bila wazo la hisia hiyo. Huwezi kuwa na hisia fulani bila kuanza kuwa na wazo lake kwanza au bila wazo lake kuwepo kwanza.
  8. Unaweza kubadili mtazamo, wazo, fikra kwa kuweka mtazamo kwenye fikra unayotaka na ile fikra ya zamani kuondoka yenyewe kwa kutawaliwa na fikra mpya.
  9. Like attracts like.
  10. Mawazo sio kitu cha kupuuzia.
Kumbuka sheria za Akili haziangalii unajua sheria hizo au haujui, hazibagui wewe ni nani, hazina utofauti na matokeo na hutokea automatically.


Vitu vya kuweka akilini na kushikialia. 
Ni vyema kujaribu mwenyewe na kuangalia je kuna ukweli wowote. Unaposoma na kuacha kama ilivyo au unaposikia na kuacha kama ilivyo au kujaribu mara moja sio sahihi. Jaribu kuweka mwaka mmoja, kwa kujichunguza mawazo yako, imani yako, fikra na msimamo wako, matendo yako na maneno yako. Chunguza kwa kina, tazama ulimwengu wa nje na uhusiano uliopo na ulimwengu wa ndani na jaribu kurekebisha fikra zako, mitazamo na kujipima utagundua mengi zaidi.

Leo hii unaweza ukaona ni kitu cha ajabu, lakini amini nakuambia kuwa elimu hii hapo kale haikupatikana huru kama hivi. Ni elimu iliyokuwa inafundishwa kwa siri, mafumbo na wapo waliokuwa wanachomwa moto kusema haya. 

Pia cha mwisho ninapenda sana kuwasisitiza, tujichunguze kwa kina ndani yetu, tutambue uridhi tulio nao kujitambua, kuweka mawazo, matendo na maneno sahii. Tutumie akili yetu kuendelea zaidi badala ya kuendelea kuwa watumwa. Baada ya kujitambua ndipo tutatambua ukuu wa ulimwengu na tutatambua ni kwanini tumeumbwa kwa sura na mfano wake yeye aliye INFINITY.