Fikra na Mawazo Mabaya Yanavyoadhiri Maisha Yetu.

Posted by Apolinary Macha on 00:00 with No comments

Miili yetu ina umeme au nguvu ambayo inaizunguka na inasimamiwa vikubwa na akili na ufahamu wetu. Nguvu hiyo inategemeana na Afya, Hisia, Mawazo, na kila wakati hubadilika badilika kutegemea na hali iliyopo katika mwili. Ni suala la kisayansi na sio la kufikirika. Miili yetu imezungukwa na energy ambayo ipo katika mawimbi mbalimbali yanayotegemeana na hali ya mwili ilivyo. Mfano mwili wenye afya mawimbi yake ya energy au nguvu kani yapo tofauti na mwili ambao hauna afya, vilevile mwili wenye hisia au fikra fulani nao pia una mawimbi yake ambayo nayo hutegemeana na hisia iliyopo. Kwenye hali ya furaha kuna aina ya mawimbi yanakuzunguka na kwenye hali ya wasiwasi au kwenye hali ya kuwa na wazo lolote baya au hali yoyote mbaya nayo inabadilisha nguvu ya mwili inayokuzunguka. Kazi ya nguvu hii ni kulinda mwili na kusambaza ujumbe katika hali ya mawimbi kwenye kila kona ya mwili.

Ufuatao ni mchoro wa kisayansi uliofanywa na Dr. Gary Young ukionyesha aina mbalimbali za mawimbi kutegemeana na hali ya mwili.


Katika mchoro huo utaona kuwa mwili wa kawaida ambao hauna matatizo unaweza kuwa na zaidi ya 68Hz ya mawimbi yanayomzunguka. Mtu mwenye kuumwa mfano kansa ana mawimbi yanayomzunguka 42Hz au zaidi na ukiwa na mawazo au fikra hasi unakuwa unapunguza mawimbi -12Hz na ukiwa na mawazo chanya unakuwa umeongeza mawimbi +10Hz. Hivyo mawimbi yetu yanachangiwa na hali ya miili yetu pamoja na hali ya Akili na ufahamu wetu.

Ni kwanini watu wengi hushikiliwa mawazo yao hasa mawazo mabaya badala ya kushikilia mawazo mazuri?