Rahisisha Maisha yako kwa kusema Ahsante

Posted by Naamini Yonazi on 14:58 with No comments
Ni muhimu kusema asante kwenyena mashaka, wasiwasi, ukikoselewa, ukiwa na hasira, au hata unapopewa pongezi au ushauri. 

Wengi wetu hatuna mazoea ya kusema ahsante isipokuwa pale tunapopokea kitu (zawadi) au pale tunapoonewa huruma kuhusu jambo fulani. 

Neno "Ahsante" hudharaulika sana na kuchukuliwa poa (under-appreciated) sana katika maongezi yetu ya kila siku. Tuangalie hali tofauti ambazo watu hutakiwa kusema Ahsante lakini husema vingine.


1. Sema Ahsante unapopokea pongezi


Mara nyingi tunadhoofisha pongezi kwa kupotosha taarifa au kwa kuwa wanyenyekevu kupita kiasi. Ukiangalia kiundani, unaweza kufikiri kwamba hii inakuzuia kuonekana kama unakiburi. Kwa kusema tu "Ahsante" inamtambua kikamilifu mtu aliyefanya pongezi na kukuwezesha kufurahia huo wakati. Kuna kitu kinachokuwezesha na kujihisi furaha pale unapokubali shukrani. 

Mfano: "Jamani umependeza!! Nimependa ulivyovaa leo"
Badala ya kusema: "Ahh! hii nguo.. mbona ya zamani! Ishapauka kwanza"
Jaribu kusema: "oh! Ahsante sana!! Nimefurahi umeipenda"


2. Shukuru pale unapochelewa


Kuchelewa ni kitu kibaya sana. Inampa mtu shida na mawazo kwa mchelewaji lakini huonyesha kutokumheshimu zaidi anayekusubiri. 

Mfano: "umechelewa dakika 15 kwenye mkutano"
Badala ya kusema: "Nisamehe nimechelewa. Kulikuwa na foleni sana leo. Sijui kwanini!"
Jaribu kusema: "Ahsante sana kwa uvumilivu na kunisubiri"

Tunapofanya kosa kama hili, fahamu kwamba mtu mwingine anasacrifice zaidi kuliko wewe. Jibu la kawaida ni kuomba msamaha na kujitetea, tunajisahau kuona pia anayetusubiri naye anabidi afikiriwe. Shukuru licha ya makosa yako.

3. Sema "Ahsante" unapomtuliza mtu.


Mtu anapokuja kwako na habari mbaya, inaweza kukufanya usijisikie vizuri. Unataka kuwa rafiki mwema lakini hujui uanzaje.

Mfano: "Mama wa rafiki yako amefariki, au kaka yako kafukuzwa kazi"
Badala ya kusema: "Angalau umejifunza mengi kutoka kwa mama.. au bora uhai wako, kazi utapata mbona!!"
Jaribu kusema: "Asante kwa kushirikiana hizi habari na mimi. Najua hii ni wakati mgumu kwako, niko kwa ajili yako"

Wakati wa mateso, mara nyingine, hatuhitaji kusikia maneno ili kupunguza maumivu kama vile tunahitaji mtu kugawana maumivu yetu.

4. Sema "Ahsante" unapopokea maoni ya manufaa.

Maoni yanaweza kuwa na manufaa sana, lakini ni mara chache sisi tunaona hivyo. Mara nyingi tunachukulia vibaya. Hakuna mtu anapenda kushindwa, lakini kushindwa ni hatua tunayopitia. Jibu kwa maoni ya msaada na shukrani na uitumie ili iwe bora zaidi wakati mwingine.

Mfano: "Hii kazi sio nzuri. Nilitegemea utafanya vyema zaidi"
Badala ya kusema: "Hapana boss sio hivyo, hichi ndicho kilichotokea..."
Jaribu kusema: "Asante kwa kutarajia zaidi yangu. Nitajitahidi"

5. Sema "Ahsante" unapopokea upinzani usiofaa au kukukosoa.

Shukuru mtu anayekukosoa. Ni vigumu sana lakini inawezekana. Wengi tunaanza kujazwa na hasira hata kabla mtu hajamaliza kuongea ili kujielezea. Mwishoni inakuwa ugomvi. Unaposhukuru mtu kwa kukukosoa, hii husababisha uwepesi wa nguvu za kauli zao.

Mfano: "Jambo ulilolisema ni la kipuuzi na la kusikitisha nililolisoma wiki hii yote."
Badala ya kusema: "Mpuuzi mwenyewe, wacha nikuambie.."
Jaribu kusema: "Ahsante kwa maoni. Bado najifunza."

6. Sema "Ahsante" wakati mtu anakupa ushauri usioombwa.

Hii hutokea mtu anapokuwa kwenye sehemu za starehe mfano gym au sehemu ya kula. Kila mtu atakuwa na maoni juu ya jinsi mbinu utakayotumia. Ukianza kula kwa mkono, unaweza kusemwa. Ukisema ufike gym uanze na vyuma, lazima kuna watu watasema. Mbinu bora ni kusema "Ahsante". Kuelezea makosa ya wengine, hayawezi kuondoa yako.

Mfano: "Umeweka video yako mtandaoni ukiwa unafanya mazoezi"

Badala ya kusema: "aahh kumbe! Wewe tuma video yako nione inavyotakiwa"
Jaribu kusema: "Ahsante kwa maoni na msaada"



Muhimu ni kusema ahsante kwenye hali zozote zile. Ukiwa na mashaka, wasiwasi, hofu, hasira nk. Ni sahihi na rahisi katika karibu hali yoyote na ni jibu bora kusema "Ahsante" kuliko mambo mengi tunayosema.

Je! Una wasiwasi kuwa muaminifu katika kuonyesha shukrani nyingi kwa watu katika maisha yako?