Umeshawahi kuchunguza kinachoendelea akilini mwako?

Posted by Apolinary Macha on 17:33 with No comments


Umeshawahi kuongea na nafsi yako kibinafsi? Umeshawahi kujaribu kuchunguza kinachoendelea akilini mwako? Mfano kuchunguza unawaza nini? Ni wazo la aina gani? Mara nyngi unawaza nini? Kuna wakati unakuta unawaza mawazo mabaya na unaweza ukajisemea mwenyewe "Acha kuwaza mawazo mabaya, hayana umuhimu" huku ukijiambia mwenyewe. Unaweza kuwa makini na mawazo yako na kuyauliza kama unavyouliza mtu mwingine au kuyachunguza kama unavyochunguza hali ya nje.

Kushindwa Kuwa makini na Jambo.
Tunaposhindwa kuelewa jambo kwa kina wengi hujikuta wanaweka fikra duni na kushikiliwa na mawazo hasi. Tunaposhindwa kuelewa hali iliyopo basi tunaweza kuzidi kutawaliwa na wasiwasi, hasira, ujinga n.k lakini tukielewa jambo au hali kwa uhalisia wa pande zote mbili yaani kwa upande unaotetea na upande unaopinga au kwa upande hasi na upande chanya tunaweza kufanya maamuzi sahihi na kutoshikiliwa na mawazo bila kujiongoza.

Badili wazo au Fikra mbaya kwa Kuipa Fikra nzuri/chanya kipaumbele.
Huwezi kuondoa mawazo au fikra mbaya kwa fikra mbaya bali vyote hivyo huondolewa kwa fikra nzuri. Mfano unapoona hasira inakutawala, ili kuiondoa hasira weka mtazamo wako kwenye upendo na hasira yenyewe itaondoka bila kipingamizi. Ibadili hasira kwa kutanguliza upendo na hasira yenyewe itaondoka kwani hakuna upendo unaokaa na hasira. Kama vile hakuna giza linalokaa na mwanga ndivyo hakuna mawazo au fikra mbaya inayoweza kukaa na fikra nzuri. Fikra nzuri huondoa fikra mbaya na mawazo mazuri huyaondoa mawazo mabaya.

Ni vyema kujitawala kwa kinachoendelea akilini na kukishinda badala ya kukiruhusu kitoke katika ulimwengu wa nje. Na ndio maana wengi hujifunza meditation/taamuli kuweza kujizoesha kujitawala na kutawala hisia zao.

Hisia/Hali za kuziepuka katika Kujitambua.
  • Hasira
  • Chuki
  • Ubinafsi
  • Wasiwasi
  • Kutojitawala
  • Uvivu na Uzembe
  • na kadhalika