Sheria ya Pili: Sheria ya Uhuru wa Fikra
Posted by Apolinary Macha on 15:13 with No comments
Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal Laws
Sheria ya Pili ya Akili na Ulimwengu - Sheria ya Uhuru wa Kufikiria.
Ni kutoka katika mada ya kwanza iliyokuwa inaelekeza umuhimu wa akili, mawazo na imani katika kuumba uhalisia wa maisha yetu. Baada ya kuelewa kuwa kuna uhusiano kati ya Akili na Wazo katika maisha yetu sheria hii ya pili kuielewa sio taabu kwani kila mmoja anafahamu hivyo.
Kusoma Sheria ya Kwanza BONYEZA HAPA.
Muamuzi mkuu ni Wewe. |
Hakuna mnyama anayeweza kuwaza anachotaka, wanyama huongozwa na hisia, hormones, insticts n.k lakini hawawezi kufanya uhuru wa maamuzi ulio nao wewe mwanadamu. Ni maajabu makubwa na ni baraka. Japokuwa hakuna anayejua ni kwanini hivyo, hakuna anayejua ni kwanini kazaliwa mawanadamu, bali tunachojua ni kuwa sisi ni wanadamu na tuna upekee mkuu sana katika utajiri tulionao na uwezo wetu wa kuyaelewa maisha kiundani zaidi ya aina nyingine zote za maisha. Nimesema aina zote za maisha kumaanisha mimea, wanyama, wadudu n.k kwani wote hao pia wana uhali, lakini hawana uhuru wa kutumia akili yao watakavyo.
Baada ya kuelewa ufahamu huu, utajikuta hausemi kuwa "ninafikra fulani kwa sababu nimefundishwa hivyo", au mwingine kuamini kitu fulani kwa sababu wazazi wamemfundisha, au marafiki, vikundi cya watu, na kadhalika. Wewe ndiye mwenye maamuzi, hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako zaidi yako wewe mwenyewe. Watu au hali zinaweza kukuhamasisha tu lakini haziwezi kukufanyia maamuzi. Hata katika imani zinazoamini Kuwa kuna shetani, hazifundishi kuwa shetani anaweza kukufanyia maamuzi bali wewe mwenyewe ndio muamuzi.
Kitu chochote unaweza kukitumia katika usahihi au katika ubaya, hata akili ya mwanadamu inaweza kutumika katika usahihi au katika ubaya. |
Kwa kuhitimisha ni kuwa, sheria hii inatusaidia kufahamu kuwa wewe ndiye mwenye maamuzi makuu katika utumiaji wa ufahamu wako. Utakavyotumia ufahamu wako ndivyo uhalisia wako utakavyokwepo. Ufahamu wako unaumba dunia/ulimwengu wako hivyo ni vyema kutumia uhuru huu kutengeneza uhalisia wako uupendao. Una uwezo wa kuamua unachotaka kufikiria. Kama unaona unafikiria mawazo mabaya sana, wasiwasi, matatizo, shida, unaweza kubadili mtazamo wako na kuwaza ya muhimu na kushukuru kwa kila hali badala ya kuumia na hali. Haijalishi mambo yanayokuzunguka ni magumu kiasi gani, haijalishi una mawazo kiasi gani, kinachojalisha ni kuwa una uhuru wa kuwaza na kuelekeza fikra yako unapopenda na fahamu kuwa popote utakapoelekeza fikra zako panakua na kufanyika uumbaji. Kujizoesha kuweka fikra ni kama aina nyingine za ujuzi, kama unavyoweza kujifunza kusoma, kuandika, n.k pia hata kujua kuongoza ufahamu na fikra yako ni mazoea tu. Ni kujizoesha kuwaza fikra fulani na mwishowe fikra hiyo inakukaa na unaweza kutumia uhuru wako utakavyo.
Akili ni kama farasi pori, ni vigumu kumuelewa lakini ukiweza kujenga urafiki naye na kumuongoza, ana nguvu kubwa katika kukusaidia lakini ukishindwa kumuongoza atakuendesha bila wewe kujijua.
0 maoni:
Chapisha Maoni