Hatua za Kuwa Na Furaha.
Posted by Apolinary Macha on 01:30 with No comments
Furaha, unaitamani. Kila mmoja wetu anatafuta furaha katika maisha yake, lakini wanadamu tunatofautiana jinsi ya kuelewa maana ya furaha ni nini.
Kuna furaha ya kweli na furaha ya uongo (furaha ambayo unaamini ni ya kweli lakini kumbe si ya kweli).
Fahamu kuwa unaweza kujitengenezea furaha wewe mwenyewe. Furaha sio inapatikana ukitimiza au kufanikisha jambo Fulani bali furaha ni maamuzi ya mtu. Amini kuwa katika kila hali, na bila kujalisha una hali gani au una nini; tambua kuwa furaha inaanza pale utakapoamua kuwa na furaha. Ni maamuzi na sio hali. Unaweza kuamua.
- Fahamu maana ya furaha.
Kwanza kabisa ili uweze kuwa na furaha tambua furaha ni nini, tambua furaha ya kweli na furaha ya uongo. Ukichunguza kila mtu anahitaji kuwa na furaha, lakini ni wachache waliowahi kujiuliza maana ya furaha ni nini.
Unaweza ukawa unapenda kusema “nikipata kitu fulani nitakuwa na furaha”, au nikiwa Fulani nitakuwa na furaha” n.k Kila mmoja ana furaha yake hivyo maana ya furaha kwa kuangalia furaha inapatikana vipi ndio maana ambayo wengi hufahamu.
Furaha – Ni hali ya hisia ambayo ikiisha tunaitamani tena, na pale itokeapo tunatamani hali hiyo iendelee. Ni vigumu sana kuelezea maana moja ya furaha lakini hali hiyo ya hisia lazima iwepo katika furaha. Na kama hamna furaha ni kutokana na hali ya kukosa hali Fulani/kitu Fulani au jambo Fulani ndipo hali ya kutokuwa na furaha inakuja. Mfano kama unaumwa hautakuwa na furaha kwani umekosa hali afya. Hivyo afya ndio chanzo cha furaha yako. Mfano unaweza ukawa hauna furaha kwa sababu umekosa upendo kwa mtu n.k
Hivyo ni vyema kufahamu furaha yako inatokana na nini. Huwezi kusema unatamani kuwa na furaha wakati haujajua furaha yako inatokana na nini/hali gani.
- Tambua kuwa kuwa na furaha ni maamuzi yako.
Kuwa na furaha haijalishi una hali gani bali unaweza ukawa na furaha wakati utakapoamua. Wengi wanapenda kusema nikipata kitu Fulani nitakuwa na furaha. Ni kutokana na kuwa wanatafuta furaha nje ya nafsi zao. Furaha ya vitu, mali, ufahari, sifa n.k ni furaha zitokazo nje yetu. Ni furaha ambazo ni za kujitengenezea na kuziamini kama ni furaha.
Kuna msemo unasema
Nje ya tajiri asiye na furaha kuna masikini mwenye furaha.
Ni msemo ulianza kutumika China katika miaka ya zamani kuonyesha kuwa sio lazima uwe na hali/kitu Fulani ndio unakuwa na furaha. Kuna ambaye hana hali/kitu hicho na ana furaha Zaidi yako.
Katika safari yako badala ya kuitafuta furaha, kuwa na furaha. Hisi furaha, shukuru kwa kila jambo, tazama mtazamo chanya na utaona furaha inazidi kuongezeka kwako. Unaweza ukapuuzia lakini ukiamua kujaribu utaona maajabu yake.
- Jifunze kuwa na furaha.
Kuwa na furaha ni hali ambayo unaweza kujifunza. Ni kweli kuwa tunapitia mambo mengi kwenye maisha, tunapoteza tunaowapenda kwa kifo n.k, tunaumwa, tunapoteza vitu vya muhimu, hasira, uovu n.k vyote hivi vina adhari katika furaha zetu lakini tunaweza kujifunza kuwa na furaha. Kama unavyojifunza kuogelea au kuendesha gari unaweza kujifunza furaha na ukaiongeza katika maisha yako bila kujali hali uliyonayo.
Acha kipindi cha wakati mgumu kipite, kishukuru kipindi hicho kwa kukusaidia kukufanya uwe mgumu Zaidi kiroho, weka Imani juu ya Muumba wako, Waza mawazo chanya, Kuwa na fikra safi, Weka matumaini, Usikubali kuanguka na shikilia penye ukweli na haki.
- Chagua kuwa na furaha hivi sasa.
Tumia wakati wa kuwa peke yako, jiangalie moyoni kama una furaha, tambua tatizo ni nini, weka malengo ya kuwa na furaha na kutimiza mipango yako na amini.
Ya Ziada.
Kumbuka kuwa kila mwanadamu anatafuta furaha, heshimu mwanadamu mwenzio na viumbe, tambua furaha yao na uwasaidie watu kutimiza furaha yako, Hiyo inazidi kukuongezea furaha na kusafisha Karma yako.
Tendea wenzio ambayo ungependa kutendewa.
0 maoni:
Chapisha Maoni