Je sayansi inasemaje kuhusiana na Uhalisia Tunaouona? Nini undani wa vitu (Matter).
Posted by Apolinary Macha on 14:24 with No comments
Uhalisia au reality ni sawa na kufahamu undani wa kitu kwa kina zaidi ya ulivyozoea kukitazama. Mfano unapofahamu uhalisia wa kitu fulani ni kwamba
Unajua chanzo cha kitu hicho, Unajua hali zote za kitu hicho na kutambua vilivyounda kitu au hali hiyo unayoiona ni uhalisia.
Lakini kwenye sayansi tunaposema uhalisia tunamaanisha kwenda ndani kabisa ya kitu fulani au object na kufahamu object hiyo imetengenezwa na nini na ndani ya vilivyotengeneza kuna nini, nacho kimetokana na nini, kazi yake, utofauti wake na kadhalika.
Kilichopo ndani ya vitu. |
Chengachenga ya Chumvi ikitazamwa kwa ndani kabisa imetokana na Neutrons na Protons kama chengachenga za vitu vingine zilivyo nazo zimetokana na Neurons na Protons. |
Zamani kuna waliokuwa wanaamini kuwa dunia ni flat na sio duara. Walikuwa wanachukulia dunia kama meza na hawakufahamu kuwa unaweza kuizunguka dunia kwa kwenda moja kwa moja katika line moja. Lakini bado kulikwepo watu ambao walikuwa wanaamini kuwa dunia ni duara. Kutokana na kuzunguka kwa mitumbwi na meli kipindi cha ubepari na kukua kwa viwanda walipokuja kufahamu kuwa ukizunguka katika direction moja kwa moja unaweza kurudi karibu na direction hiyo na ndipo walipokuja kuangalia umbo ambalo inawezekana dunia inalo ni umbo la duara au umbo la yai lakini wakawa hawaamini kuwa dunia ni flat tena. Baada ya ugunduzi wa satelite na kurusha camera nje ya dunia tunafahamu kuwa kumbe dunia ni duara.
Hivyo uhalisia hubadilika na labda tunachoona leo ni kweli kwa miaka ijayo inawezekana kuwa sio kweli.
UCHUNGUZI MKUU WA SASA.
Uchunguzi mkuu wa sasa unatumia Quantum Physics katika kuelewa ulimwengu. Ulimwengu ni infinite na hauna mpaka na hakuna anayeweza kuumaliza kwa kuufahamu hivyo wanasansi wanajitahidi kutaka kufahamu nini kinachounda vitu tunavyiviona.Miaka ya zamani waliweza kuamini kuwa Ulimwengu muunganiko wa material ya aina kuu nne na hupatikana kila mahali na kila kimoja kilichopo ulimwenguni kina sifa mojawapo ya hivi vitu
- Moto,
- Maji,
- Hewa,
- Na Ardhi/Udongo.
Mchoro wa kiBuddhism unaiotwa Mandala, ukionyesha hali kuu nne za matter yaani Hewa/Upepo, Udongo/Ardhi, Moto na Maji. |
Lakini sayansi ya sasa haijabishana na uelewa huo ila ukaona kuwa hivyo sio inavyounda matter (vitu) bali vinavyounda vitu ni elements. Na hizo elements nne ni makundi ya elements na matter.
Hivi sasa inaaminika kuwa kila matter ina atom. Lakini ndani ya atom kuna Nucleus na ndani ya kiini cha Atom hamna kitu zaidi ya energy (umeme).
Kiini (Protons na Neutrons) na Electrons. |
Mpaka hapo utakuwa umepata picha kuwa kila kilichopo duniani na ulimwenguni kimetokana na energy. Asilimia kuwa ya matter ni sehemu isiyo na nafasi.
Unaweza ukashangaa sana endapo ukija kufahamu ukweli huu kuwa kila kitu duniani ni energy na unachokiona ni vibration ya vitu mbalimbali katika energy mbalimbali na ndio maana unaona kitu fulani ni tofauti na kingine ni kwasababu kinachovitofautisha ni energy iliyopo ndani yake na jinsi inavyo vibrate.
Kila kitu ndani yake ni Enegy ndiyo imeunda Kiini chake. Kila kiini ni umeme. |
Ukitaka kuuelewa ulimwengu fahamu kuwa kila kitu ni umeme, kila unachokiona ndani yake kiini chake ni umeme, kila sauti unayosikia ni mtetemeko wa umeme, kila hisia unayohisi ni aina ya umeme inayopita kwenye mishipa ya damu, tunapokula ni kwamba chakula ni matter ambayo miili yetu inaweza kuchukua energy inayopatikana kwenye kiini cha chakula (matter ya chakula), na kubadilisha kuwa nguvu kani na mwili kuutumia. Na miili tukishaiacha nayo inabadilika na kuwa matter na kurudi kama chengachenga za dunia na baadaye hubadilishwa kuwa chakula tena. Mimea kazi yake ni kunyonya chenga chenga za matter zinazounda uhali (energy ya mwili wa kiumbe) na kubadilisha kuwa chakula na viumbe na aina nyingine zote za uhai hutegemea hicho.
Sawa na Umeme |
Pia kila wazo, hisia, neno, tendo na kadhalika ni energy na kila kimoja hakipotei bure. Kwani energy haiwezi kuharibiwa bali inaweza kubadilishwa kutoka aina moja ya energy kwenda nyingine na ndio maana ulimwengu ni infinite.
0 maoni:
Chapisha Maoni