Sheria ya Tatu - Sheria ya Nguvu ya Umakini/Focus
Posted by Apolinary Macha on 12:21 with 3 comments
Kanuni ya Tatu - Sheria ya Umakini.
Bado tupo katika sheria kuu kumi ambazo zina uwezo mkubwa kwa mwanadamu katika kujitambua na kufahamu zaidi maajabu ya ulimwengu.
Sheria ya kwanza ilikuwa inasema kuwa ili kitu kuwepo au hali kuwepo lazima kuwepo kuwa sababu yake. Kwa maana kuwa hakuna tokeo lisilo na chanzo. Kila hali ina chanzo chake kinachopelekea hali hiyo kuwepo, kila kitu kuwepo lazima kuwe kuna chanzo chake kupelekea kuwepo. La si hivyo kisingekwepo.
Katika ulimwengu wa akili, ufahamu na ulimwengu tukaona kuwa chanzo kikuu cha ufahamu ni akili. Mawazo huweza kufanyiwa kazi na kupelekea kuumbwa kwa kilichokuwa kinawazwa. Tukachukulia mfano computer, simu, madirisha, mavazi n.k vyote hivi vilianza kama wazo, idea halafu vikafanyiwa nguvu kazi na vikatokea katika ulimwengu wa kifizikia.
BONYEZA HAPA KUSOMA SHERIA YA KWANZA
BONYEZA HAPA KUSOMA SHERIA YA KWANZA
Sheria ya pili ilikuwa inasema kuwa tuna uwezo wa kuelekeza mtazamo wetu popote tutakapo. Unaweza kuamua kuwaza unachotaka kuwaza, unaweza kuamini unachotaka kuamini, unaweza kuamua uelewe nini na ukatae nini. Ni uhuru wa Free Will katika kufikiria. Una uhuru wa kufikiria unachotaka na hakuna anayeweza kufikiria katika akili yako bali wewe mwenyewe.
BONYEZA HAPA KUSOMA SHERIA YA PILI
BONYEZA HAPA KUSOMA SHERIA YA PILI
Sheria ya tatu ndio ambayo nitaielezea kwa undani zaidi.
SHERIA YA NGUVU YA UMAKINI.
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua, kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.
UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa pamoja.
Mwalimu mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa:
Umakini ni kama mwanga wa jua, unauona ni wa kawaida lakini ukiweka lensi mbinuko unaukusanya mwanga ule na kuwasha moto.
Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona tamaduni za kiAsia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo nguvu hiyo huamka.
Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni mimi pale nilipokuwa najifunza Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza kutengeneza.
Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo. Sheria hii kiini chake kipo hivi.
POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani n.k utaona ufahamu uo unakua. Buddha aliwahi kusema hivi,
Chochote unachoweka umakini hukua. |
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana, halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri. Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au Nature imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya Nature, na hata akili ni nature hivyo ipo mpaka kwenye fikra, mawazo, misimamo n.k
Mfamo unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe reality yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu kuwa kuna sheria kama hii duniani.
Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini. Je ni kweli reality yako imetokana na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona hivyo au ni reality?
Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu. Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi, ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe. Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe. Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu unaohukumu hali na sio hali yenyewe.
Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu inaumba ulimwengu wa nje.
Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine. Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO.
MIFANO:
Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona.
Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa na akili. KUna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza kuona dalili.
Categories: Amka, Furaha, Happiness, Jitambue, Kuamka, Kujitambua, Mafanikio, Mambo ya Muhimu, Mawazo, Ndoto na Malengo, Ufahamu, Wazo
Uko vizuri Bro
JibuFutaKiungo cha sheria no2 mbona kinakuludisha kwenye sheria yakwanza
JibuFutaLakin pia tunasubiria shelia ya4
JibuFuta