Kanuni ya nne - Sheria ya Upekee wa Uelewa na Uhalisia wa Maisha
Posted by Apolinary Macha on 15:04 with No comments
Kanuni za Akili na Ulimwengu.
Kanuni ya nne - Sheria ya Upekee wa Uelewa na Uhalisia wa Maisha
Maisha unayoishi hivi sasa hayajaachana na ulimwengu unaoendelea akilini. Ukiwa umefuatilia sheria ya kwanza utakuwa umejifunza kuwa kila tokeo lina chanzo chake, sheria ya pili ikasema mwanadamu ana uhuru wa kufikiria na ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kutumia akili yake kufikiria na sio mwingine, kila mmoja ana uhuru wa kufikiria na kanuni ya tatu ikasema kuwa unapoelekeza umakini wako napo panakua.
Sheria au kanuni hii ya nne inafuata baada ya kuelewa kanuni zile tatu zilizotangulia. Kanuni zote zimeonyesha umuhimu wa akili na ufahamu wetu katika kutengeneza maisha yetu. Sheria hii ni kama imedhibitisha kabisa kwa kusema kuwa uhalisia wa kila mwanadamu unatokana na kinachoendelea kwenye akili yake.
Ulimwengu wa ndani unahusisha mengi sana, unahusisha imani yako juu ya maisha, uelewa wako juu ya maisha, jinsi unavyoona na kuweka mtazamo wako katika mawazo, fikra na hali mbalimbali, wasiwasi, hisia (mbaya na nzuri), mawazo ya ndani ya kujisemea mwenyewe, matendo yako utendayo ndani na nje ya ufahamu wako n.k
Kila mwanadamu, kila mtu, anaishi katika uelewa wake juu ya ulimwengu huu. Hii ndio maana, kila mmoja ana Nature of Reality yake (Uhalisia wake). Kila mtu anaishi katika dunia yake pekee na maalum kwa upande wake. Kwa mara ya kwanza unaweza ukashangaa kuona ufahamu huu lakini ukizidi kuuweka akilini na kuutafakari kwa kutazama maisha na watu mbalimbali utaona kuna ukweli mkubwa sana ambao ni wachache wameweza kuugundua na kuona jinsi kanuni hii inavyofanya kazi katika maisha yetu.
Kutokana na sheria hii inamaanisha kuwa wanadamu wanatofautiana sana juu ya uhalisia walio nao wa ulimwengu, kila mtu ana uhalisia wake na tafsiri yake ya ndani. Lakini utofauti huo ukiuchunguza utagundua umetokana na utofauti wa akili na matumizi ya ufahamu kwa kila mtu.
MIFANO.
Bugs: Huu ni mtazamo walio nao watu wanaoitazama dunia kifizikia. Maisha yao yanatokana na uelewa wao unaopatikana katika milango ya ufahamu, aina hii ya watu inategemea milango ya ufahamu kuelewa ulimwengu huu. Wengi wao huamini kuwa maisha yanatokea tu, hamna chanzo cha hali walizonazo wala hamna chanzo cha matokeo wanayoyaona wao huona matokeo ni matokeo tu na hawawazii kama kunaweza kukawa na chanzo, hawawazi kuwa kuna ulimwengu wa ndani bali wao huishi kwa kutazama ulimwengu wa nje na kuona upo tu kama ulivyo. Watu hawa huweka mitazamo yao katika kuamini bila kufuatilia chanzo kwani aina hii ya watu hutegemea dunia ya nje.
Watesekaji - Hawa pia nao wanaishi katika uelewa wao wa uhalisia wa maisha. Hawa hutumia ufahamu wao kuweka umakini kwenye pande mbili mbili za maisha. Kila wanachoona wanaona kuna sides mbili, wanaona kuna pande mbili mbili. Aina hii ya watu wameweza kuendeleza ufahamu wao kwa kuona kuna mema na mabaya, mazuri na mabaya, mwanga na giza, shetani na Mungu, chuki na upendo, afya na magonjwa, umasikini na utajiri. Yaani kila wanachokiona lazima waona kinyume chake. Aina hii ya watu hujikita sana katika imani na kuona kila jambo lina pande yake na wanahukumu kuwa upande fulani ndio mbaya na huu ndio mzuri. Hupoteza wakati wao kuona hiki ni kema na kingine ni kibaya badala ya kufuatilia ni kwanini. Aina hii ya watu huweka judgements na ni wepesi kuhukumu.
Wengi wao huamini kuwa Mungu ndiye mpaji, na wanaamini kuwa wakikaa katika mazuri watapata mazuri na wakikaa katika mabaya Mungu atawahukumu na kuwateketeza.
Waabuduji- Hawa huamini kuwa baraka na mikosi inatoka nje yao. Hawa hawaamini kuwa maisha yao yanahamasika na wao bali wao huamini kuwa maisha yao yameundwa na hali au na chanzo ambacho wao hawawezi kukiongoza. Wao huweka imani zao nje yao. Wengi huamini mambo ya kuridhi, utabiri wa nyota, jinsia, miaka, rangi za mwili, na elimu zao ndio peke yake vinatengeneza maisha ya watu. Wengine huamini kabisa race/aina fulani ya watu ina akili zaidi yao. Pia huamini kuwa mambo yanayotokea katika maisha yao huadhiriwa na rangi walizovaa, au mafuta wanayojipaka, harufu na manukato wanayotumia, anachoambiwa na walimu wake au na jamii, waganga wa jadi, vyakula wanavyokula, mpangilio wa nyumba na jinsi wanavyolala, nyota, majina, miaka ya kuzaliwa n.k Kwa kifupi aina hii ya watu huamini dunia ya nje yao ndio inapangilia maisha yao.
Wapanda Milima - Aina hii ya fikra ni aina ambayo wanadamu wengi wa aina hii wameonekana kama watu waliofanikiwa katika maisha. Hawa huamini kuwa wana nguvu ya asili ndani yao katika kutengeneza maisha yao. Wanaamini uwezo wao, akili zao na juhudi zao katika maisha. NI aina ya watu ambao waliwahi kutamani kutimiza jambo fulani, wakajitahidi katika maisha yao kulitimiza, japokuwa waliona changamoto lakini hawakuweka akili zao kwenye kushindwa bali walizidi kuamini nguvu ya ndani na hatimaye wakafanikiwa malengo yao na kuona umuhimu wa kuwa na imani na kuwaza mawazo chanya. Na baada ya kufanikiwa malengo yao hawa wanajitahidi kuhamasisha wengine kujituma na kuwashauri wajaribu kuanda milima au vikwazo walivyo navyo kwa imani ya kujiamini. Hawa huishia kuwa wabunifu wakuu wa vitu mbali mbali, n.k
Wapanda Milima |
Waamini - Hawa ni wale wanaoamini kuwa kuna Supreme Master lakini hawashikiliwi na kulazimika kuamini katika dini. Hawa huamini huisoma dunia ya kiimani na dunia ya kifizikia kwa pamoja kuelewa ulimwengu. Hawa huona maisha ni mageuzi na kila siku jamii zinazidi kuwa na akili na wanaamini hapo baadaye mwanadamu atazidi kubadilika na kuzidisha akili na huona kuwa maisha ni maajabu na wao hutumia maisha yao kujifunza siri za maisha. Hawa hawana sifa ya kuamini tu kila jambo bali wanapenda kulichunguza na kupenda kujua mengi. Wengi hufikia hatua ya kufunuliwa na kuamka baada ya kufahamu sana Nature of Reality (Uhalisia).
Mgawanyiko huo haujalenga kuwagawanya watu mbali mbali katika mitazamo yao bali ni kama mfano kuonyesha kuwa wanadamu wanaishi katika tafsiri yake tofauti tofauti juu ya ulimwengu. Na tafsiri hizo zinaadhari maisha yetu.
Kanuni hii ni mwanga kwani inakusaidia kuzidi kujichunguza na kuchagua mtazamo ambao umejifunza na kuuchunguza badala ya kuamini tu kila jambo. Ufahamu kuwa unachoamini na kufahamu juu ya maisha hakina umbali na maisha yako. Ni kama gurudumu.
Categories: Enlightenment, Jitambue, Kuamka, Kujitambua, Mafanikio, Mafunzo, Maisha, Malengo, Mambo ya Muhimu, Mipango, Ndoto na Malengo, Ufahamu
0 maoni:
Chapisha Maoni