Kanuni ya Tano: Upekee wa Fikra na Uhalisia wa Maisha Yako

Posted by Apolinary Macha on 15:33 with No comments

 Kila mwanadamu ni mwakilishi wa ufahamu mkuu wa ulimwengu tunaoishi.

Kila mwanadamu ni mwakilishi wa ufahamu mkuu wa ulimwengu tunaoishi. Kila utofauti wa mtu una nafasi yake katika ulimwengu kwani kila mtu au kila ufahamu unawakilisha ufahamu mkuu wa ulimwengu. Kama unakumbuka kuna mojawapo ya Sheria ambazo niliwahi kuzielezea hii ni mojawapo kati ya muendelezo wako juu ya akili na ufahamu kwa ujumla. 

Tulipata kufahamu kuwa kila mwanadamu anaishi katika uelewa wake na ufahamu wake, na ufahamu huo una mchango mkubwa sana katika kutengeneza maisha ya mtu anayeamini au anayeishi katika mfumo huo. Kama unakumbuka kuwa sheria zilizotangulia zimeonyesha jinsi ufahamu unavyounda maisha yetu. Wazo sio kitu cha kuchukulia kawaida, wazo linaweza kufanyiwa uumbaji na likatokea katika ulimwengu wa kifizikia. Kila mtu anaishi katika uhalisia wake ambao hauna umbali na ufahamu na uelewa wake juu ya maisha kwa ujumla. 

Ujumbe mkuu katika sheria hii ni kuwa: Kama kila mwanadamu anaishi katika ulimwengu wake kutokana na ufahamu wake, chochote unachofikiri ulimwengu ulivyo katika tafsiri uelewayo wewe, ndivyo ulimwengu ulivyo katika uhalisia WAKO. 

Quantum Physics inafundisha kuwa tunaishi katika ulimwengu wa energy na energy hiyo ni sawa na ufahamu. Kumbuka kuwa wazo ni umeme, na haka katika sayansi inasema pia kuwa dunia tunayoishi ni umeme kwani kila kitu kimetokana na energy. Ukichunguza kila kitu kinachotuzunguka ikiwa ni simu, miti, mawe, computer, nyumba na kadhalika vyote hivyo ukivichunguza kwa darubini kali utagundua vyote vimeundwa na Atom, Atom  ukiichunguza kwa microscope nzuri utagundua kuwa inaundwa na  na chenga chenga za sub-atomic na chenga chenga hizo ndogo saaaaaaana kuona kwa macho ni field of energy (Ni kama duara ndani yake kuna umeme/energy).

Katika uelewa hii tunasema kuwa kila kitu ni sehemu ya ufahamu wetu. Ukitaa kubadili ulimwengu wako badili ufahamu wako juu ya ulimwengu huo na utaona kuwa kila kitu kinabadilika kuendana na ufahamu mpya. Sheria hii inatufundisha kuwa wewe ni sehemu pekee ya ufahamu na wewe ndiye sehemu ambayo ni makao makuu ya ufahamu wako na ufahamu wako ni makao makuu ya ufahamu mkuu wa ulimwengu kwani ulimwengu nao una ufahamu wake mkuu ambao ndio ufahamu wa asilia. 

Sehemu yako ya ufahamu ni sehemu ya pekee sana kwani ni kiwakilishi cha ufahamu mkuu na pia ni sehemu ya ufahamu mkuu wa ulimwengu kwa pamoja. Wewe ni sehemu ambayo hiyo energy field inatengenezwa na kuumbwa.

Ujumbe wa sheria hii ni: Kama haupendi maisha unayoishi katika huu ufahamu wako, unaweza kuyabadili kwa kubadili umakini wako (Focus/Awareness)