Kanuni ya Sita: Kanuni ya Uumbaji.
Posted by Apolinary Macha on 17:23 with No comments
Kila wazo, Kila neno, Kila tendo, ni kama sala. |
Kutokana na kuwa kila wakati kuna kinachoendelea katika ufahamu wako basi tambua kuwa kila wakati kuna uumbaji unaendelea katika ulimwengu wako/Uhalisia au Reality yako.
Tumeweza kujifunza katika sheria ambazo zimepita kuwa kuna uhalisia, mawazo, akili, ulimwengu, illusion, n.k na vyote hivi vinatofautiana kati ya mtu na mtu na ndio maana experience yetu na uelewa wetu juu ya maisha haufanani kwani kila mmoja anatofautiana na mwenziye kwa hivyo. Tumeweza kufahamu kuwa uumbaji unaendelea na kila tendo tutendalo ni kuumba kile kilichopo katika ufahamu wetu na sio kingine. Mfano tunatengeneza magari ambayo kabla ya kutengenezwa hapo mwanzo ni mtu au watu walikaa na kuwaza, kisha wakafanyia juhudi au tendo na wazo likabadilika na kutoka katika hali ya wazo na kuwa uhalisia. Leo hii tunaweza kusema kuwa miaka kumi iliyopita hatukuwahi kusema au kutegemea kuwa kungekwepo na teknolojia hii ya sasa mfano aina za simu, lakini hatufahamu ndani ya mwanadamu mwingine kuna nini, unaweza kukuta idea au wazo la yule aliyetengeneza hapo mwanzo lilikuwa ni wazo na kama asingelitendea kazi lisingefanyika, na kumbe wazo na action lazima vifuatane kupelekea wazo kuwa katika matokeo.
Unaweza ukaona kama ni mada ya ajabu kwani hapo mwanzo hukuwahi kuwaza ni kwanini watu wanakumbwa na maisha tofauti tofauti na kila mmoja anatumia maisha yake kitofauti lakini jibu tunalipata katika Fikra ya mtu ilivyo na matendo ya mtu yalivyo. Fikra ni kiini na tendo ni kifuniko cha kiini kinacholinda kiini na kukisaidia kitokee. Ukipenda kuelewa sana kuhusiana na hili jichunguze kwa kina sana kwa kujiangalia unaamini nini, nenda deep ndani kabisa na ukubali pale nafsi inapokuambia kuwa umedanganya kwani kuna wakati watu hujilazimisha kujifanya hawaelewi majibu ya ndani ya nafsi ambayo ni majibu kutoka kwa Ufahamu mkuu wa Ulimwengu huu.
TURUDI KATIKA MADA KWA KINA:
Watu wengi sana hawafahamu kuwa wanatawaliwa na akili zao, hisia zao na mawazo yao, na ndio maana wengi wanayatazama maisha katika hali ambayo hawaridhiki nayo. Lakini ni nani wa kumlaumu? Wao wenyewe hawafahamu hilo na wanaona ni kawaida labda maisha au Mungu amewapangia hivyo.
Ndio maana wengine hukata tamaa sana, wengine hawawezi kuacha addictions, mazoea, tamaa huwatawala, hisia (hisia hasa mbaya), na kujikuta wanalaumu hali za nje yao kama vile watu, maisha, shetani, uchawi, majirani n.k.
Kila mtu ambaye amekuwa mwalimu mzuri wa kuigwa na anayeweza kuwahamasisha watu waweze kutimiza malengo yao huwaimiza sana kuweka mawazo chanya, kuweka mawazo chanya ni kuelekeza ufahamu wako katika hali ya juu zaidi na kubadili uhalisia wako.
Sheria ya Uumbaji ni sheria ambayo nayo inazungumzia hasa kuwa kila wakati tunawaza jambo na kulitenda tunalibadilisha kutoka katika hali isiyo ya kifizikia (wazo, energy, umeme) kuwa katika hali ya kifizikia au hali ya milango ya ufahamu na kukiona katika experience ya milango ya ufahamu lakini hapo kabla kinakuwa katika sehemu ya ufahamu na akili.
Wengi tunafahamu kuwa ulimwengu wa sasa umeweka sehemu kubwa ya utafiti katika Quantum Physics, mafundisho ya meditation na yoga, na saikolojia kwani wamegundua kuwa vyote vilivyopo nje vimetoka ndani. Akili ya mtu inaweza kubuni kitu na mtu akakitendea kazi kikatokea katika ulimwengu wa kiuhalisia na kuwahamasisha na wanadamu wengine. Ndio maana wanahimiza kuifahamu nature ya consciousness ili kuielewa reality.
Categories: Enlightenment, Fikra, Happiness, Jitambue, Kuamka, Mambo ya Muhimu, Mawazo, Meditation, Ufahamu, Utulivu, Yoga na Meditation
0 maoni:
Chapisha Maoni