Jinsi ya Kutuliza Akili Kwenye Meditation (Tamuli)
Posted by Apolinary Macha on 14:05 with 2 comments
Meditation
au taamuli ni kitendo ambacho wengi ambao wamejifunza mambo mengi ya hekima,
nguvu ya akili katika maisha ya mwanadamu, sayansi, na Imani mbalimbali,
wamekuwa wakivutiwa na kufanya meditation. Mojawapo ya changamoto ya kwanza
ambayo wengi wamekuwa wakikutana nayo ni akili kuhama sana kwenye meditation.
Kupitia Makala hii, nitajaribu kuelezea njia mbalimbali ambazo unaweza
kuzifanya katika kuhakikisha akili inatulia sehemu moja na kuongeza nguvu ya
umakini na utambuzi wa hali ya akili yako.
Mwanzo
Meditation au kwa jina la kiswahi Taamuli
ni kitendo cha kutazama hali (nature) ya akili na kuongeza utambuzi na umakini.
Wengi wanaofanya meditation ni kwa lengo la kuituliza akili kutoka katika
stress, msongo wa mawazo, kuongeza hekima, kuongeza umakini na utambuzi juu ya
mtu binafsi na jinsi alivyo. Pia wengine hufanya meditation kuachana na
addictions na mazoea na kuongeza willi-power. Na wapo wanaofanya meditation
kuongeza uwezo wa sheria ya usumaku (law of attraction) na wengine hufanya
meditation kuongeza umakini, ubunifu (mfano wachoraji, wanamuziki, wasomi n.k).
Kuna sababu nyingi ambazo kila mtu binafsi anaamua kufanya meditation.
Akili ni kitu ambacho ni kitu Tata sana
(very complex). Ni sehemu ya mwanadamu ambayo haijagunduliwa vyema jinsi
ifanyavyo kazi na hakuna mtu anayeweza kukusaidia kufikiri au kujua jinsi akili
yako ifanyavyo kazi. Mara nyingi tumekuwa watumwa wa akili zetu bila kutambua
kuwa tunaweza kutawala akili zetu na kuamuru akili iwaze nini, isiwaze chochote
au kuamua kuweka umakini katika jambo Fulani kwa jinsi utakavyo wewe. Akili
ukiweza kuiongoza utakusaidia lakini ukishindwa utakuwa mtumwa wake utakuwa
mtumwa daima. Ndipo utakuta hali kama addictions, mazoea mabaya, umakini,
hekima na uvumilivu tunashindwa kuwa navyo kwa sababu hatuwezi kutumia akili
zetu ipasavyo.
Tatizo linalosababisha akili kutotulia
Kwa kawaida tangu unapoamka na mpaka
unapoenda kulala akili inafanya kazi. Kila wakati utawaza hichi, kisha utawaza
kingine, na ukitaka kujua hilo chukua kalamu na karatasi na saa. Andika kwenye
karatasi kila kitu au wazo au hisia itakayopita akilini. Mfano ukiwaza kuhusu
kazini andika kwenye karatasi “kazini”, ukimuwaza mtu andika jina lake, andika
kwa ufupi ili upate muda wa kuandika. Hakikisha umeandika kila kitu na kisha
baada ya dakika kumi utaona ni mawazo au hisia nyingi zimepita akili. Huo ni
mfano tu kuwa kwa kawaida akili huwa haitulii. Itawaza hichi, itakumbuka ya
jana, utakuwa na hisia Fulani, na kila hali inakuja na kupita. Ndivyo
tulivyozoea maishani.
Meditation na Akili.
Kwenye meditation unajifunza kuitawala na
kuingoza akili kwa dakika Fulani. Mfano meditation ya Samadhi Meditation ambayo
unaiweka akili katika umakini mmoja tu; ni kitendo cha kuelekeza akili katika
jambo moja au kitu kimoja mfano kwenye pumzi tu. Kila saa na kila dakika
tunapumua, lakini hatuweki akili zetu kwenye pumzi kwa sababu haina umuhimu
kutazama pumzi kila saa. Hivyo meditation ya kuongoza akili inatumia pumzi kwa
sababu ni hali ambayo wakati wote tunayo, haiitaji kuwasha mshumaa au kutazama
kitu Fulani. Kuweka akili kwenye pumzi ni cheap/rahisi na haiitaji chochote. Ni
mtu tu mwenyewe kutumia pumzi na kujaribu kuiweka akili sehemu moja kwa dakika
chache. Unaweza kufanya meditation kwa kuweka akili yako kwenye mshumaa,
kutazama bahari, kutazama chochote unachokiamini n.k. Kwa hapa leo
nitazungumzia kuitawala akili kwenye pumzi.
Ukiwa unafanya meditation
Ukiwa unafanya meditation unakaa mkao ambao
utakuwa huru na utaweza kukaa kwa dakika chache bila kuhama. Unaweza kukaa
kwenye kiti lakini usilale kwa sababu unaweza ukasinzia kutokana na uvivu. Pia
kama unaweza kukunja miguu kwa muda mrefu pia unaweza kukaa vizuri chini, juu
ta mto au kitu ambacho kitaepusha maumivu ukikaa sakafuni.
Ukianza hakikisha hutasumbuliwa na utapata
muda wa dakika chache kukaa peke yako. Pia unaweza kufanya meditation na
wengine kwa kukaa pamoja na kila mmoja kuangalia upande wake (ili kuwa na
concentration/umakini). Kwa wanaoanza tumia dakika 10. Kila wiki unaweza
kuongeza dakika 5 mfano 15, halafu wiki ijayo ukajifunza 20 na kisha zoea
kutawala akili kwa dakika 20 kila siku ndani ya mwezi mmoja na baadae unaweza
kutumia 30 mpaka 40, sio lazima uzidi 40, cha msingi sio dakika ni umakini ndio
uongeze. chukua saa au simu ikukumbushe dakika kumi zikifika. Hakikisha umeweka
simu silent, na ukiwa kwenye meditation usiangalie zimebaki dakika ngapi,
dedicate kuwa na subira mpaka muda utimie.
Ukianza weka akili kwenye pumzi, vuta pumzi
taratibu na weka break kisha toa pumzi taratibu. Yaani unavuta pumzi, unakaa
kidooogo kisha unaitoa taaratibu huku ukitazama jinsi hewa inavyoingia puani na
kifua kikitanuka na hewa ikitoka na kifua kikishuka taaratibu. Ukigundua akili
haipo tena kwenye pumzi usijali wala usijilaumu au kuona umekosea, ni kitendo
cha kawaida akili kuhama bila kujijua. Cha msingi irudishe tena akili kwenye
pumzi kama mwazoni. Endelea hivyo hivyo. Akili ikihama unairudisha kwenye
pumzi. Ukiona kama unarelax na unahisi mwili umetulia sana huwa kuna kama raha Fulani
unaihisi au umeme/waves Fulani ya relaxation unaiona unakuzunguka achana nayo
na usiweke akili kwenye raha inayokujia ukiwa unafanya meditation wewe endelea
kuweka akili kwenye pumzi na ile raha itaendelea kuwepo. Ukiiwaza utapotea, ni
kama mtego.
Akili ikiwa haitulii.
Samahani kwa kuanza kuelezea mengi kwa
sababu hapa ndipo kwenye mada kuu. Nilipenda kutoa introduction kwa ambao
hawajui ili wafahamu na tuende sawa.
Akili huwa kwa mara ya kwanza kufanya
meditation inahama sana. Sio tatizo ni hali ya kawaida. Ni udhibitisho kuwa
akili inahitaji kutulizwa. Kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya. Unaweza
kuhesabu pumzi inapoingia. Ukahesabu Moja….mbili…tatu na kufika kumi kisha rudi
tisa, nane, saba, sita….. mpaka sifuri kisha anza tena moja, mbili…na
kuendelea.
Njia nyingine, ukiona akili inahama, mfano
unawaza kuhusu jambo Fulani, sema kwa taratibu “akili najua unawaza kuhusu
masuala ya kazini, rudi kwenye pumzi”. Kusema hivyo sio kwamba unaongea na
akili bali inakupa mazoea ya kujua kinachoendelea akili na kukifanyia maamuzi.
Ukiona unawaza kuhusu kitu Fulani mfano pesa zako ulipoziweka sema “akili najua
unawaza pesa zangu, rudi kwenye pumzi” kisha endelea kuweka umakini kwenye
pumzi.
Baada ya kufanya meditation mara kwa mara
utaona kuhama kwa akili kumepungua na unaanza kuona raha kufanya meditation.
Pia baada ya meditation utakuwa unahisi Amani na kama ulikuwa umeshusha mzigo
mzito akilini. Pia katika maisha utakuwa makini na kinachoendelea akilini mwako
na kukusaidia kujitambua vyema.
Asante.
Thank you ! Ntaanza kujaribu kufanya Meditation
JibuFutaMinaomba niulize kwani tamuli na jichola3 nki2ki1 au v2tofauti
JibuFuta