Imani duni Zinazorudisha Nyuma Ndoto na Malengo
Posted by Apolinary Macha on 12:43 with No comments
Kumbuka malengo yako kila siku na yape kipaumbele - Paulo Coelho.
Una ndoto na malengo, kila mtu ana malengo na ndoto zake anazofikiria kuzifikia. Kama hauna malengo au mipango utabakiwa kuwa sawa na mtu asiyejua anapaswa kufanya nini.
Umeshawahi kujiuliza "Ni kwanini nimezaliwa? Ninapaswa nifanye nini?" Ni dhahiri kuwa haujazaliwa kwa bahati mbaya, umekuja duniani na kupewa akili kwa sababu maalum. Ni vyema kutumia maisha yetu vyema kwa kuchagua malengo sahihi na yanayoendana na sababu na vipaji vyetu katika kuangaza ulimwengu na kuwahamasisha wanadamu wengine kutimiza mwangazao wapo pia.
Unaweza ukawa na mipango yako na malengo lakini usifahamu cha kufanya au kutoamini kabisa kwamba unaweza kutimiza malengo yako.
IMANI ZETU HUUMBA UHALISIA WETU.
Mawazo yetu, fikra zetu, misimamo yetu, ufahamu na uelewa wetu una adhari kubwa katika maisha yetu. Kwa vyote hivyo vinatusaidia kufanya maamuzi, na kila siku mwanadamu hufanya maamuzi. Kufanya maamuzi hupelekea kubadili maisha yetu kabisa. Kila siku kuna maamuzi mbalimbali unayoamua mfano aina ya chakula cha kula, jinsi ya kutumia kipato, watu wa kuongea nao, nini cha kuongea nao na kadhalika na vyote hivi hubadili sehemu fulani katika maisha yetu.
Zifuatazo ni imani zinazoweza kukurudisha nyuma katika kufikia malengo yako:
+Imani ya kuona ni Vigumu sana kutimiza malengo yako,
Unaweza ukawa na malengo yako lakini ndani yako kuna imani ya kuamini kuwa malengo yako ni vigumu sana kuyatimiza. Kama unafikiri malengo yako ni vigumu sana kutimiza jiulize, ni njia gani ndogo ndogo zinazoweza kukusaidia taaratibu kutimiza malengo yako? Tambua kuwa maisha yanaweza kubadilika katika sekunde moja na kubadili maisha yako kwa ujumla. Fikiria mwaka jana siku kama hii na muda kama huu ulikwepo wapi? Je ulitegemea ungefika hapa? Je ulitegemea leo hii ungekuwa hivi? Fikiria miaka 10 au 5 iliyopita bado utaona kuwa maisha yanabadilika sana. Hakuna kilicho kigumu bali ugumu upo kwenye imani yako. Fanya unachokipenda hata kama kwa dakika tano tu kilasiku kifanye.
Kama unapenda kuwa mwanariadha tumia dakika tano kukimbia na kufanya mazoezi,
Kama unapenda kuwa muandishi, tumia hata muda mchache kila siku kujifunza chochote kuhusiana na uandishi,
Kama unapenda kuanzisha biashara kubwa tumia muda kila siku kutazama biashara za wengine, jifunze biashara zinaendaje na weka urafiki na wafanyabiashara,
Kama unapenda kitu fulani na unapenda kutimiza malengo yako kupitia unachokipenda tumia muda kufanya unachokipenda hata kwa dakika chache, itakusaidia kujijenga kiimani kuwa unaweza kutimiza na pia itakuandaa siku maisha yakikupa nafasi kutimiza malengo yako tayari una msingi mzuri kuishi katika ndoto zako, BADALA YA KUKAA NA KUONA NI VIGUMU KUTIMIZA NDOTO ZAKO TUMIA MUDA MACHACHE UJIFUNZE KITU KUPITIA NDOTO ZAKO NA IPO SIKU ZITAKUJA UKISHAJENGA IMANI KUWA UNAWEZA.
+Imani ya kuamini kuwa ni lazima ufanikiwe haraka haraka,
Hata ulimwengu ulichukua miaka na miaka kubadilika na leo hii unauona. Tazama Nature, haina haraka, lakini lazima kila kitu kikamilike. Mbegu taaratibu huanza kukua kwenye udongo mchafu, mbegu huumia kwa kupasuka ganda lake ambalo lilikuwa ni kinga yake, na mbegu ikajifunza kuufuata mwanga na mpaka imetokeza nje ya udongo na kuw mti mkubwa.
Hakuna kutegemea mambo haraka haraka, Maisha yanapenda tuwe wavumilivu na tukishikilia imani kuwa ipo siku ndoto zitafika pale unapotaka ziwe. Somo la kwanza au jaribu la kwanza ambalo maisha hutufunza ni KUWA WAVUMILIVU.
+Imani ya kuona ni lazima uwe maarufu,
Hakuna umaarufu unaokuja tu, bali inapaswa mtu kufanya anachokipenda, akikitimiza na kuwahamasisha wanadamu wengine katika kazi yake basi umaarufu kwake ni lazima kama vile kivuli kinachokufuata. Umaarufu sio kitu cha kukikimbilia au kukitamani bali weka nia kwenye malengo na ndoto zako, kupitia malengo na ndoto zako zikifika mbali na kuziongoza vyema furaha yake ni bora kuliko kutaka umaarufu.
+Imani ya kuona nimechelewa sana kuishi katika ndoto zangu,
Wapo watu wanaofanya kazi maofisini na ni watu wazima na umri wao ni mkubwa lakini hapendi wanachokifanya, labda alikuwa anatamani kuwa na kazi fulani na kazi aliyonayo anaifanya kwa malengo ya pesa, hao nao huteseka sana. Ni heri kutumia wiki moja kuishi katika ndoto zako badala ya kutumia miaka 100 ukiishi katika mazingira na hali usiyoipenda. Ni taabu ni ni mateso. Usikubali siku unalala na umebakia muda mchache wa maisha yako kuisha halafu unajiuliza ni nini umefanya katika maisha yako, inauma sana. Ni vyema kutoona umechelewa na badala yake ishi katika malengo yako na yatimize ili safari yako ya maisha itakapoisha uwe umeyatumia maisha yako vyema.
+Imani ya kuona ni Hatari sana.
Hii ni sawa na hofu, mtu huogopa kutimiza anachokitaka au malengo yake kwani anaogopa. Hofu hurudisha nyuma imani na hukosesha amani. Ni vyema kuitawala hofu kwa kuongea matumaini.
0 maoni:
Chapisha Maoni