Ni Wakati wa Kuanza Mwaka kwa Furaha
Posted by Apolinary Macha on 16:18 with 1 comment
"Mojawapo ya jambo muhimu sana katika maisha yetu ni kufurahia maisha - Kuwa na furaha - Ndio jambo la muhimu" Audrey Hepburn
Kila mwanadamu anapenda kuwa na furaha, furaha ni lengo la muhimu sana kwenye maisha yetu sisi wanadamu. Kama ilivyo kawaida kwa watu wengi, kila mmoja anapenda kuwa na siku yenye furaha, wiki yenye furaha, mwezi wenye furaha na mwaka wenye furaha. Wanadamu tunaweka sheria mbalimbali za kuishi ili tuishi kwa amani na furaha, tunajituma na biashara na kazi ili tuwe na maisha mazuri yenye furaha. Tunaishi na watu vyema ikiwemo ndugu zetu na wanafamilia ili tuwe na amani na furaha. Kila tunachokifanya katika maisha yetu tunalenga kuwa na furaha.
Tukisema tuweze kuchambua sana kuhusiana na jinsi tunavyoitafuta furaha, ni mlolongo mrefu na mifano mingi tunaweza kupata katika kuchambua lengo la furaha na maisha ya wanadamu. Lakini mbali na yote, tunaanza mwaka mpya na ni vyema tukumbuke mambo machache katika kutafuta furaha yetu ya maisha.
Weka Fikra na Kipaumbele Ambapo Panakupa Furaha
Kila siku, ni nafasi yetu kuamua kuwa na furaha au kutokuwa na furaha. Katika kila jambo na katika kila hali tunaweza kuchagua kuwa na furaha au kuwa na fikra katika upande mbaya wa hasi. Ukichunguza vizuri katika maisha yetu, bila kujali mtu unapata taabu gani za maisha; lazima utapata kitu ambacho kinakupa furaha. Hakuna mwanadamu ambaye ana taabu kwa asilimia zote.Unapoanza mwaka upya, weka nia ya kuhakikisha kuwa unaweka kipaumbele katika nafasi, watu , hali, vitu au chochote kinachokupa furaha. Acha kushikilia huzuni na majuto bali weka akili yako kwenye furaha. Chukulia mwaka mpya ni nafasi ya kuanza mwaka kwa furaha na chunguza kinachokupa furaha kisha kipe kipaumbele.
Nimeienda hii mada
JibuFuta