Kwanini ni Vyema Kushukuru kwa Kila Hali Uliyonayo Sasa?

Posted by Apolinary Macha on 23:30 with No comments
Gratitudes
Siku moja mfalme fulani alimwendea mwalimu wa imani na aliyekuwa na busara sana. Mfalme akamuuliza “Ninapotazama wafuasi wako naona wapo vizuri na mpaka Ngozi zao. Pia nimesikia kwamba wanakula mlo mmoja tu kwa siku, lakini kwa kweli nashindwa kuelewa wanaweza vipi kuudumisha mwenendo huu wa maisha.”
Mwalimu akamjibu “Wanafunzi wangu hawayajutii matendo waliyofanya zamani isipokuwa wanajitahidi zaidi na zaidi kutenda matendo mema. Siyo kwa kujuta, kusali na kuabudu isipokuwa kwa kuwasaidia wengine ndio watu watu wanaweza kufanya toba kwa makosa waliyoyafanya zamani. Wafuasi wangu hawana wasiwasi kuhusu mambo yatakayowafikia baadaye. Wanatosheka na chochote wanachopata na kwa hiyo wanadumu katika hali ya kutosheka. Hawaoni kama hiki au kile hakitoshi, huo ndio mtindo wa maisha yao kwa hiyo wanaweza kuidumisha amani ya maisha yao kwa kutosheka.”
Mtu yoyote anaweza kuudumisha huu uchangamfu kwa kutosheka. Kama mtu akiuliza kwa nini hatuna furaha katika maisha yetuingawa vitu tulivyonavyo ni zaidi ya mahitaji yetu, ni njia gani sahihi ya kumjibu?  Jibu sahihi ni kwa sababu hatutosheki. Kama tungetosheka, tusingesema kwamba hiki au kile ni pungufu. Hatuwezi kutosheka kwa ajili kuna upinzania kati ya hamu zetu za kibinafsi ambazo hazina kikomo na sheria ya kutodumu kwa vitu.
Moja kati ya ushauri ambao walimu wengi wa kiimani wamekuwa wakituhamasisha ni kuwa “Kutosheka ni utajiri mkubwa kuliko aina yoyote ya utajiri”.
Mtu tajiri haina maana kwamba anacho kila kitu,mtu tajiri naye pia kila wakati anahofia usalama wake. Bado naye ana majukumu ya kulinda woga wake. Bado naye atatawaliwa na fikra za woga na wasiwasi, akifikiria kwamba watu wanamsubiri kumdhulumu. Tajiri hawezi kutoka nje bila usalama, hawezi hata kulala mlango wazi na uhuru mwingine hana. Utaona wote masikini na tajiri bado wanatafuta na kutorishika na walichonacho. Masikini anategemea tajiri ana raha na akiwa tajiri anaanza kuwa na kazi ya kulinda alichokipata na mwishowe maisha yake yanaisha mwisho wake unafika na anaacha kila kitu cha kifizikia alichokuwa anakimiliki.
Mtu aliyetosheka na hali yake ndiye tajiri wa kweli. Mwingine anasema ametosheka na kiwango alichopata kwake na kwa familia yake, na kinachozidi anamsaidia mwanadamu mwingine naye aweze kuishi salama. Hebu pata picha ya maisha hayo ulimwengu ungekuwaje. Watu wasipoamua kuzidi tamaa za misingi na kujiwekea tamaa zao wenyewe zisizo za msingi.
Maisha ya kuridhika yanampa mtu matumaini na kumpa uwezo wa kushukuru kwa kila jambo. Unaposhukuru kwa kila jambo unakaribisha mambo ambayo utashukuru zaidi. The universe inapenda shukrani. Unaposhukuru zaidi unazidi kupata vya kushukuru zaidi. Hivyo wewe kazi yako ni kuhsukuru na kupata kila cha kushukuru.