Umuhimu wa Asubuhi Uamkapo.

Posted by Unknown on 09:05 with 1 comment
Asubuhi

Asubuhi ni muda maalum sana kwetu kwani ndio muda ambao akili inakuwa imetoka katika utulivu na Ego inakuwa bado haijaanza kukutawala. Unapoamka na mtazamo fulani na siku nzima unaikaribisha katika mtazamo huo. 

Ni vyema kuamka asubuhi kwa furaha, utaratibu, amani, na kushukuru kwa kuamka vyema na kuahidi kuitumia vyema siku yako katika maendeleo ya ndani na nje ya nafsi yako.

Wengine hutumia asubuhi kutafakari, kupangilia siku, na kuweka mipango mbalimbali ya siku nzima. Pia ni vyema kufanya meditation (taamuli) pale unapoamka kwani akili inakuwa ni tulivu na Ego bado inakuwa haijaanza kuchukua nafasi.

Jenga mazoea.

Wengi wanapoamka asubuhi wamezoea kufanya matendo fulani bila wao kujali. Mfano kuna wanaoamka asubuhi, wanapiga mswaki, wanaoga na kuvaa nguo na kisha wanaenda kwenye shughuli zao. Kila wakiamka bila kuweka umakini na ufahamu wanajikuta wakitenda kwa mazoea na sio kwa ufahamu kamili. Ni vyema kujitazama, kuweka umakini katika kila tendo unalolitenda, kuweka akili yako katika wakati uliopo na kutambua kinachoendelea katika ulimwengu wako wa ndani na ulimwengu wako wa nje.

Kuna mazoea aina mbalimbali, kuna mazoea mazuri na kuna mazoea mabaya. Kila unapoamka ni vyema kuianza siku yako katika mazoea mazuri, unaamka vyema, unasali kushukuru kwa kuamka vyema, unakunywa maji kwa afya yako, unapangilia malazi vyema kwa umakini kabisa. Unajinyoosha vyema au ukiweza kupata nafasi fanya meditation kwa muda wa Dakika 5 mpaka 10. Baada ya hapo pangilia vyema siku yako na unapenda siku ya leo ufanye nini cha umuhimu, ahadi ulizoziahidi leo za kutimiza leo na sio lazima uende sawa na ratiba ninayokuelekeza unaweza ukapanga ratiba yako nzuri, ya umuhimu, na ifuate vyema kila uamkapo. 

Jitambue Sasa
Unaweza ukatumia muda wako wa asubuhi kwa kuamka mapema na kufanya mazoezi.

Unaweza ukachagua kimoja au baadhi ya vifuatavyo katika ratiba yako ya asubuhi:
  • Kufanya Meditation,
  • Kufanya mazoezi,
  • Kusoma Kitabu cha Kukuhamasisha kujitambua,
  • Kupangilia ratiba yako ya siku na vitu vya muhimu kwa siku,
  • Kupangilia Malazi yako,
  • Kufanya Sala,
  • Kufanya Yoga,

Tumia muda wako wa Asubuhi kuipangilia siku yako vyema na kukaribisha furaha ya siku. Usiache kutanguliza Busara, Umakini, Upendo na Bidii katika shughuli zako za siku kwa kuianza siku vyema. 

Jitambue Sasa
Asubuhi