Kwanini kuna umuhimu kupata muda wa kuwa peke yako?

Posted by Apolinary Macha on 17:03 with No comments

"Kuwa peke yako kunakupa nafasi ya kujichunguza kiundani na kujitambua"

Kutokana na changamoto na mambo mbalimbali ya maisha, unaweza ukajikuta unatamani hali ya kuwa pekee. Kwanini ni muhimu kuwa pekee? Kwanini akili au mwili kuna wakati hutamani kuwa peke yake?

Hebu fikiria kila siku unapoamka mpaka unapolala, umekutana na mangapi? Umepoteza nguvu/energy ya mwili kiasi gani na katika shughuli ghani? Je ulipata muda wa kukaa peke yako na kuweza kuzungumza na nafsi yako?

Kutokana na tafiti mbalimbali, kuna umuhimu mkubwa sana pale unapotumia muda wako kukaa na kutafakari binafsi.


Kuna wakati unaweza ukawa umebanwa na mambo mengi, mawazo, hasira au vitu kukuzonga na kutamani kukaa peke yako na kutafakari, ni jambo la muhimu kwani kutafakari peke yako kunaweza kukusaidia mambo mbalimbali kama vile:
  • Kujitambua
  • Kujua hisia zako mfano kama una hasira itapoa n.k
  • Kupumzisha akili kutokana na mambo mengi.
  • Kubadilisha mawazo na fikra yako
  • Kuongeza kipaji katika kazi za ubunifu
  • Kuongeza uwezo wa kufikiri na kutazama mambo mbalimbali katika fikra mbalimbali. Mafano huepusha kufanya maamuzi hasa katika hali mbaya mfano asira au katika msongo wa mawazo.
  • Huepusha kujitazama vibaya, huongeza kujiamini na kujitambua.
  • Na pia inasaidia kutambua asili ya mawazo yako na jinsi unavyopokea mawazo/thoughts kutoka akilini.
Kila siku ni muhimu kutumia muda (hata kama ni kwa muda mfupi) kuwa peke yako na kuongea na nafsi yako.

Nakutakia furaha na amani daima. 


Categories: