Hali Tatu Za Maisha Ya Binadamu.
Posted by Apolinary Macha on 19:36 with No comments
Watakatifu huwekewa alama ya mwanga juu ya kichwa kumaanisha ameweza kufungua Chakra ya Utosini. Na hupokea Energy kutoka katika Chakra kuu ya ulimwengu. |
Kila mwanadamu ana hali tatu au tabia tatu, yaani
- Hali ya Mnyama
- Hali ya Ubinadamu
- na Hali ya Utakatifu.
Wanyama hawana njia ya kuzimiliki tabia zao za kinyama kwa sababu wanatawaliwa zaidi na hisia. Lakini tukiwa kama binadamu, kwa kutumia akili zetu kuchambua na kufikiri, mambo mengine ambayo sio sawa au sawa au kuangalia mambo ya muhimu katika maisha yetu na kuangalia manufaa ya furaha ya wanadamu wengine. Uwezo huu alio nao mwanadamu ndio tofauti kubwa kati yake na wanyama. Manadamu anaweza kutumia akili yake na kuiongoza. Pia mwanadamu anaukweli tayari ndani mwake, hatawaliwi na hisia za mwili au za milango ya fahamu bali kwa jicho la tatu au jicho la kiimani.
Kwa kudhibiti tabia zetu za kinyama, kwa kuacha unyang'anyi au uporaji, kwa kuendeleza urafiki na huruma, tunaongezza subira, uvumilivu, maelewano, umoja na ushirikiano na nia njema. Hizi ni tabia za asili za kiutu. Ni tabia ambazo tunazo ndani yetu, haiitaji vitabu vya kidini wala mwalimu wa kidini kuzitambua tabia njema. Tunazo tayari ndani mwetu, tunachopaswa ni kuziishi.
Lengo la mmsingi wa dini mbalimbali ni kuzikuza hizi tabia njema, lakini lazima tuelewe kwamba baadhi ya tabia hizo zimo ndani yetu tayari. Akili ya mwanadamu inaweza kufunzwa kufuata njia njema na kuishi katika haki au pia unaweza ukashindwa kuiongoza akili yako na kuwa mtumwa wa akili yako. Wapo wanadamu mbalimbali maisha wanayoyaishi ni kama wanyama, hawawezi kuongoza hisia zao, hawawezi kujitawala kitabia, uovu umewazoea na wao wamezoea uovu. Na inakuwa ni ngumu sana kwao kuweza kujibadilisha kutokana na maisha wanayoishi.
Hivyo tunapaswa kufahamu kuwa sisi wanadamu tunayo nafasi ya kuishi kama wanyama, wanadamu na watakatifu. Kila haki inazoeleka na tunaweza kujifunza kuishi na kubadilika kutoka hali mbaya au duni kimaisha kwa
- Kujifunza ukweli wa maisha
- Kutambua sisi ni nani,
- Kutambua akili yako ipoje,
- Kujifunza imani na kufuata njia njema,
- Kuishi katika haki,
- Kufanya Meditation au Yoga,
- Kujifunza kutawala milango yetu ya hisia,
- na Kuongoza akili yetu badala ya kuiacha ituongoze.
0 maoni:
Chapisha Maoni