Jifunze kuitazama na kuichunguza mitazamo yako.
Posted by Unknown on 09:47 with No comments
Jifunze kuitazama mitazamo yako. |
Hii ikiwa na maana kuwa maisha jinsi yanavyokulea, ni kutokana na jinsi unavyoyatazama na si vingine. Watu wengi hawajawahi kujichunguza kiundani, na kuchunguza maisha yao kwa nje. Ndio maana inapelekea watu wachache kuelewa ufahamu huu na kuukubali kwani inabidi UJITAMBUE kwanza ndipo utatambua maisha ni kwanini yanakutokea kama yalivyo.
Quantum Physics au elimu ya kuchunguza chembechembe za matter(vitu), inasema kuwa kila kitu katika ulimwengu ni Energy (nguvu kani). Kila kitu, sauti, wazo, tendo, kila kitu kinachoshikika na kisichoshikika kina energy na energy ndiyo inayokishikilia na kukitofautisha na kingine. Ufahamu pia ni energy, ndani yake kuna energy mbalimbali zinazotoka kama vile mawazo, fikra, hisia, mtazamo, na energy hiyo hutoka nje katika hali ya tendo na kutimizika kwake hufuatia.
Ndio maana inaaminika kuwa Ulimwengu wa nje unatokana na ulimwengu wa ndani. Kila kitu kimetokana na Ufahamu. Ufahamu ni sehemu ya pekee ya uumbaji na hakuna anayefahamu ufahamu umetokana na nini na umeanzaje. Kila kitu kinatazamwa na ufahamu fulani ili kuwepo. Sio kila kitu kimetokana na ufahamu wako. Kuna vitu vimetokana na ufahamu mkuu. Ufahamu huu mkuu umepelekea uumbaji wa Ulimwengu huu kwani ndio uliokuwa wa kwanza kuutazama ulimwengu na kuunda. Ufahamu huu mkuu umekuwa ukiitwa majina tofauti tofauti, Ufahamu mkuu wengine wamekuwa wakiuita Mungu bila kufahamu Mungu ni nani. Sheria za ulimwengu kama vile nguvu ya mvutano, na kadhalika ambazo mwanadamu hawezi kuzibadili zimetoka katika ufahamu mkuu. Mwanadamu sio ufahamu mkuu lakini ni ufahamu unaojitegemea uliounganika na ufahamu mkuu. Ndani yako una ufahamu wako lakini umeungana na ufahamu mkuu. Ndani yako kuna nguvu kubwa na kabla maisha haya hayajaanza ilikwepo, na hata maisha haya ya mwili yakipita itakwepo na itazidi kuwepo. Ni elimu ambayo ina undani sana lakini inahitaji mtu kutafuta na kujifunza zaidi kwa kujichunguza.
Hata Yesu alisema kuwa, "Laiti kama mwanadamu akiwa na imani hata kidogo kama chenga ya haradani anaweza kuhamisha mlima kwa kutoa amri". Pia aliowaponyesha aliwaambia "Imani yao imewaponya".
Maana kamili ni kuwa Imani inaadhiri sana maisha yetu. Jinsi imani yako ilivyo na unachoona ni sahihi, kinakubalika katika sehemu yako kuu ya ufahamu (subconscious mind) na kinaanza kufanyiwa kazi. Tatizo ni muda, inachukua muda kuona kilichopo ndani kinatoka nje lakini pia tufahamu kuwa muda ni mazingaumbwe. Muda umetokana na mwanadamu kutazama maisha kama mlolongo wa matukio, mfano kuna jana, leo na kesho. Muda ni utofauti uliopo kati ya jana, leo na kesho. Kama kungekuwa hakuna tofauti kabisa kati ya leo, jana na kesho tusingekuwa na muda. Kama wakati uliopo utaendelea kuwepo daima na haubadiliki basi muda usingekwepo maana hakuna mabadiliko hata chembe moja na muda hautaonekana kwani hakutakuwa na ishara za mabadiliko na hatutaona utafauti wa saa moja au siku moja na nyingine. Muda umetokea kutokana na utofauti wa wakati uliopo. Maisha yanabadilika, wakati uliopo ndio wakati wa pekee na jana ilishapita na haipo tena na kesho haifahamiki itafikaje lakini ukiutumia wakati uliopo utaibadili kesho lakini kwa wakati ujao hutaweza kubadili wakati uliopo. Wakati uliopo ndio wakati mkuu wa kuweka umakini na kufahamu maisha yanataka ujifunze nini na ufahamu nini.
Hivyo weka malengo kujifahamu, chunguza unachokiamini, je kinaadhari gani katika maisha yako? Chunguza matendo yako, fikra zako, misimamo yako, maneno yako, na fahamu yana adhari gani katika maisha yako. Ukiona kuna adhari yoyote mbaya, ondoa kinachokurudisha nyuma na weka msimamo mzuri. Ondoa matendo mabaya, mawazo mabaya, fikra duni, na utaona jinsi maisha yanavyokulea.
0 maoni:
Chapisha Maoni