Sababu 4 Ambazo Zimekwamisha Mipango Ya Watu Wengi
Posted by Unknown on 11:22 with No comments
Kama una malengo Fulani katika maisha na
unapenda kufahamu ni nini kinachopelekea wengi kushindwa kutimiza malengo yao
ili kuhakikisha unaepuka kurudia makosa, hii mada inakulenga. Mada hii inajaribu
kuelezea mambo makuu ambayo wengi wanashindwa kutimiza malengo yao. Mambo haya
yamekuwa yakikwamisha wengi. Ni vyema kufahamu ili kuweza kupanga malengo na
kuyatimiza. Nitaelezea mambo makuu manne. Kuna uwezekano kuwa kuna sababu
nyingi zinazoweza kupelekea watu kushindwa kutimiza malengo yao lakini sababu
hizi nne zimechangia kwa kiasi kikubwa.
1. Mitazamo duni
Kuna wengi ambao wanashindwa kutimiza plans
na malengo mbalimbali kwanza kwa kuamini kuwa hawawezi kutimiza. Kupanga lengo
sio kwamba ndio kuamini kuwa utaweza kutimiza. Kuamini ni jambo la ndani mwa
nafsi zetu na sio kitu kirahisi kama tunavyofikiri. Inaweza pia ikatokana na
watu wamekuambia kuwa haiwezekani, labda kutokana na wao kushindwa. Inaweza
ikatokana na kuona ugumu wa kutimiza malengo yako.
Unapokuwa na imani kuwa unaweza, au unapokuwa na Imani kuwa hauwezi, katika upande wowote upo sahihi– Henry Ford
Ili kuepuka changamoto hii,
- Pasua mipango mikubwa kuwa mipango midogo midogo itakayokusaidia kufikia mipango mikubwa,
- Epuka kukata tamaa haraka,
- Kuwa na mitazamo chanya,
- Kuwa makini na angalia nafasi yoyote inayoweza kukusaidia kutimiza malengo yako na ifuate.
2.
Kupanga malengo ambayo sio
sahihi
Kuna wakati huwa
tunapenda kupanga malengo kutokana na kuiga, kutofahamu nafsi inapenda kufanya
nini, kushindwa kuangalia vipaji vyetu na nafasi tulizo nazo kufanya kitu cha
upekee. Panga malengo sahihi, kuna wakati unaweza ukawa unapanga malengo ambayo
unataka kuonyesha sifa kwa wengine, malengo ambayo huyapendi kutoka moyoni,
malengo ambayo unayapanga kwa kuiga watu, kutumia kigezo cha kushindwa kama
kigezo, kuiga mawazo ya watu bila kuangalia nafsi inataka nini.
3.
Mazoea mabaya
Hili ni mojawapo
ya tatizo ambalo kiuhalisia linawasumbua watu wengi sana. Wengi wanapanga
malengo lakini wanasahau kuwa mazoea yana nafasi kubwa sana katika maisha yetu.
Kila siku, wanadamu wanatofautiana jinsi wanavyotumia muda wao na wanavyoishi
kimazoea. Mazoea ndio yanayotenganisha waliofanikiwa malengo na wanaishindwa
kufanikiwa malengo. Mazoea kama kutumia pesa vibaya, matendo yasiyo na umuhimu
katika maisha, na mazoea yasiyo na faida ni vitu vinavyorudisha nyuma hatua za
kufika maendeleo na kufanikisha mipango katika maisha. Jenga mazoea yenye faida
katika maisha na jizoeshe kuna furaha kuishi katika mazoea hayo. Kuna watu
wanaojizoesha kufanya kazi kwa bidii, mazoea ya kutumia pesa na mali vyema,
mazoea ya kuishi na watu vizuri, mazoea ya kujisomea vitu mbalimbali, na mazoea
ya kuwa na mitazamo sahihi.
4.
Kuathiriwa na sababu za nje
yako
Katika kupanga
kutimiza malengo yetu kuna changamoto ambazo ni lazima tuzipitie, mawazo hasi
katika akili zetu lazima yawepo, watu ambao watakuambia mambo ambayo ni hasi na
kukatisha tamaa. Vikwazo na changamoto katika kutimiza mipango ni kawaida
katika maisha. Hakuna asiyekutana na changamoto. Ila jinsi unavyotazama
changamoto katika upande chanya ndipo utaweza kushindwa changamoto na kufika
mbali katika malengo.
0 maoni:
Chapisha Maoni