Wasiwasi Una Nafasi Gani Katika Maisha Yetu?
Posted by Unknown on 17:45 with No comments
Wasiwasi |
Kuna mahali paliweza kuelezea kuwa wasiwasi ni hisia (kama zilivyo hisia nyingine mfano hasira, upendo,) ambayo ina nafasi yake ya kipekee katika viungo vya mwili, ubongo na katika maisha kwa ujumla. Wasi wasi unaweza kupelekea mtu kujificha, kukimbia, kuua, kutetemeka, kubadilika na hata kufanya ambacho hukutegemea.
Wasi wasi unaanza pale unaposhindwa kuelewa uhalisia wa jambo, pale unapokuwa na hofu juu ya jambo fulani au hali fulani na kutokwepo kwa amani. Ukiwa mdogo unaweza ukawa unaangalia hata muvi ya kutisha na ukaweka wasiwasi na hofu kabisa kama vile jambo ni la kweli lakini kumbe ni muvi tu, hakuna anayekufa wala kuumia.
Katika hali yetu ya maisha, wasiwasi ni sehemu mojawapo inayotutawala. Wasiwasi juu ya mali, watoto, pesa, muda na wakati na mpaka wasi wasi unaohusisha marafiki na ndugu zetu wanaotuzunguka.
Wasiwasi huwezi kuundoa katika maisha kwani ni hisia kama hisia nyingine lakini unachopaswa ni kutokukubali wasi wasi uchukue nafasi kubwa katika maisha yako. Usikubali kuishi katika wasi wasi. Ukiwa na wasi wasi haikusaidii kwa lolote bali inakuzuia kuelewa jambo kwa uhalisia. Wasiwasi hauwezi kukusaidia kusuluhisha bali utazidi kukuogopesha. Tunapaswa kukutana uso kwa uso changamoto zote za maisha na zitazame bila woga na wasiwasi.
Wakati mwingine katika giza nene, nyota huonekana vyema na kung'aa.
0 maoni:
Chapisha Maoni