Umuhimu wa wakati uliopo (wakati wa sasa).

Posted by Apolinary Macha on 16:00 with No comments
  

Wengi tunafahamu kuwa kuna aina tatu za wakati -
  • Wakati uliopita,
  • Wakati uliopo au wakati wa sasa, na
  • wakati ujao.
 Ukiwa mdogo, kipindi ambacho ndipo unaanza kujifunza ulimwengu ulivyo, jamii inavyokufundusha na kwa kutumia milango yetu ya ufahamu tunajifunza kuwa kuna nyakati tatu.


Wakati uliopita.
Huu ni wakati ambao hauwezi kuubadilisha, hauwezi kurudisha kilichotokea wakati huu. Ubongo unahifadhi kumbukumbu za wakati huu katika neurons katika hali ya mawimbi ya umeme. Unapokuwa unajaribu kukumbuka kumbukumbu iliyopita basi Ubongo unatuma taarifa katika neorons zilizojitengeneza wakati unahifadhi kumbukumbu hiyo na hivyo kumbukumbu ni umeme uliohifadhiwa na sio uhalisia.


Wakati ujao.
Wakati ujao ni wakati ambao bado haujatokea au unaelekea kutokea. Ni wakati ambao makusudio fulani yanakwepo na wakati huu ujao unatenganishwa na wakato uliopita kwa wakati uliopo.


Wakati wa sasa au wakati uliopo.
Huu ni wakati wa muhimu sana katika maisha yetu kuliko wakati uliopita na wakati uliopo. Tambua kuwa kuna sehemu ya Ubongo isiyojua nyakati. Kitendo cha kusema kuna wakati uliopo, uliopita na ujao ni elimu inavyosema lakini hakuna ushahidi kuwa kuna wakati katika ulimwengu wa uhalisia.




Labda ili niieweke mada hii vizuri ili iweze kueleweka tutambue kuwa hakuna wakati uliopita wala wakati ujao. Wakati uliopo ndio wakati au muda pekee uliopo. Wakati uliopita umeshapita na haupo tena, wala wakati ujao ni mategemeo tu na sio uhalisia. Wakati uliopo ndio uhalisia kamili ulipo.



Kama unaweza kuishi maisha yako kwa kutumia wakati uliopo tu kuishi basi unaweza kuongoza  nyakati zote. Wakati uliopo ndio wakati wa kuuwekea fikra, kama unaweza kuutumia vyema basi unaweza ukatambua umuhimu wake.

Wengi wamekuwa wakishikiliwa na matukio, kumbukumbu na fikra za wakati uliopita au za kuwazia wakati ujao na kushindwa kuishi katika wakati uliopo. Tunapaswa kuepuka kushikiliwa na kumbukumbu za nyakati zilizopita, mfano makosa yetu, maisha yetu, watu au vitu tulivyovipoteza ambavyo havipo sasa n.k vyote hivi vinaweza kukunyima raha na badala ya kuufurahia wakati uliopo unaumia kwa kuwaza wakati ujao au uliopita.

Lengo la mada hii ni kuhimiza watu badala ya kuumia kwa mawazo au kumbukumbu za mambo yaliyopita au yanayotegemea kutokea tunapaswa tuuishi wakati uliopo. Wakati uliopo ukiweza kuuishi vyema basi wakati huu utakapokuwa ni kumbukumbu utakuwa na kumbukumbu nzuri lakini ukiendelea kuumia kwa mambo yaliyopita au yajayo hutaweza kuufurahia wakati uliopo na mwishowe wakati uliopo utakupita nao utakuwa kumbukumbu.

Mwalimu mmoja wa imani aliwahi kusema
Kama unaweza kuutumia wakati uliopo vyema basi unaweza kuuongoza wakati ujao na uliopita vyema. 

Mfano kama unautumia wakati uliopo kutenda mema na kuishi katika haki haijalishi maisha ya baadaye au baada ya kifo yapoje, lazima utategemea matokeo mazuri kwani unautumia vyema wakati uliopo. Ni sawa mna mkulima asiyepoteza muda wake kuwaza mavuno yatakuwaje bali anajitolea nguvu kazi kwa wakati uliopo (kuweka mbolea, kulima, kupanda miche bora na mbegu bora) bila kujali wakati ujao.

Unapoelekeza mawazo na fikra zao katika wakati uliopo unaweza kutumia nafasi hiyo kubadili mambo yajayo kwa kutumia mawazo yako, nguvu kazi yako, na imani yako kwa wakati huu wa sasa.