Ulimwengu wa Ndani na Ulimwengu wa Nje.

Posted by Apolinary Macha on 13:59 with No comments
Jitambue Sasa

Unaweza ukawa uliwahi kusoma mada inaelezea ulimwengu wa ndani au ukaona mahali panapoelezea kuhusu ulimwengu wa nje. Tunaposema ulimwengu wa ndani tunamaanisha ulimwengu usiotumia ufahamu wa milango ya ufahamu.

Ulimwengu wa Nje: Huu ni ulimwengu ambao mwanadamu anatumia milango ya ufahamu kuielewa. Kuna pua, masikio, ulimi, macho, na ngozi. Vyote hivi hutusaidia kupata taarifa ya mazingira yanayotuzunguka. Mfano mzuri ni kuwa tunatumia masikio ili kusikia. Je tunasikia nini? Sauti ni nini? Sauti ni mtetemeko au vibration. Mtetemeko huo tunatumia masikio kuutambua. Mtetemeko huo au vibration hizo zinapita kwenye sikio, ambapo sikio lina vimifupa vidogo sana, ambavyo vimifupa hivyo vinapeleka mtetemeko kwenye sehemu ya mwisho ya ndani ya sikio ambayo ipo kama vinyweleo vya ndani ya majimaji, vinyweleo hivyo vinatikisika pale sauti ikivifikia na vinabadili mtikisiko ule au vibration ile katika umeme. Sikio linabadili sauti kuwa umeme, umeme huo unapita kwenye neva mpaka kwenye ubongo ambapo tunapata tafsiri ya sauti.

Ulimwengu wa Nje


Milango Ya Ufahamu Tunaitumia katika Kuutambue Ulimwengu wa Nje.
 Sawa sawa na pua, ulimi, macho na kadhalika. Milango ya ufahamu inabadili taarifa na akili inatafsiri taarifa na ufahamu unakuwa mtazamaji wa akili na hisia zote.

Ulimwengu wa ndani: ni ulimwengu usiotumia milango ya ufahamu kuutambua. Ni ulimwengu mwingine kabisa. Ni ulimwengu ambao unahusisha mawazo, hisia, akili, ufahamu na utambuzi. Ulimwengu huu upo ndani yetu. Kwa mgeni wa mada hii ni fumbo kubwa sana kwake lakini kwa waliojifunza Buddhism na Mafundisho ya kiasia, Akili ni Mlango wa ufahamu. Katika buddhism akili ni mlango wa ufahamu.
Ulimwengu wa Ndani.

Ni kwanini Buddhism, Hinduism na Imani za kale zinafundisha kuwa akili nayo ni mlango wa ufahamu?
Ukiwa umelala, unaota ndoto, katika ndoto ile utaona mazingira, unaweza kusikia sauti, unaweza kuota unaongea na mtu, Je katika ndoto hiyo, macho yanakuwa hayafanyi kazi, lakini unaona, masikio hayafanyi kazi kwani unakuwa umelala lakini unaona. Ndio maana akili nayo ni mlango wa ufahamu lakini ni sehemu ambayo milango mingine ya ufahamu imekutana. Akili ipo pale milango yako ya ufahamu kulingana. Ndio maana wanafalsafa wa zamani wanaamini kuwa akili yenyewe inaweza kutumia milango ya ufahamu bila uhuru wako. Ndio maana ukilala unaona japokuwa macho yamefunga. Kumbe ulimwengu wa ndani hauna uhusiano na milango ya ufahamu. Bali kuanzia kwenye akili mpaka ufahamu ulipo ulimwengu huu ndio unapofanya kazi yake.