Kubaliana na Uzuri Wako na Ongeza Furaha Yako.

Posted by Apolinary Macha on 00:00 with No comments


Kwa sababu ya tabasamu lako, maisha yako nayo yanakuwa na furaha- Thich Nhat Hanh


Je kuna kitu cha muhimu zaidi ya furaha? Nini cha zaidi pale mtu anapokuwa na furaha? Sidhani kwani dhumuni la maisha ni kuwa na furaha na kila jambo tunalofanya ni kwa lengo la kupelekea kuwa na furaha. 

Umeshawahi kumuona mtoto ana furaha? Utaona nawe unafurahi kwa kuona furaha yake. 

Mojawapo katika vitu ambavyo watu wamekuwa wakiviangalia na wengi kuvitegemea kuwapa furaha ni muonekano wao. Umeshawahi kuona watu ambao hawana furaha kutokana na muonekano wao na wengine wanajitahidi kuweka muonekano wao katika hali ya kuwa na furaha daima?

Unaweza kujikubali katika muonekano wako na kufanya maisha yako yawe na furaha kwa kutoruhusu mawazo chanya kuweza kutawala akili yako. Kama watu wengi walivyotuahidi na kufundisha tangu enzi za zamani kuwa akili ya mwanadamu ni ya ajabu sana. Unaweza ukaifundisha kuona uzuri tu au kuona ubaya tu. Nawe pia unaweza kufungua akili yako na kuanza kujikubali katika uzuri na kuoona ubaya wake. 

Anza kujikubali. 

Kuna watu wanaamka asubuhi na kuona siku yao ni mbaya na kujiona siku hiyo wamekaa vibaya. 
Unaweza kuamka asubuhi na kuanza siku yako kwa kujitazama kwenye kioo na kuonyesha tabasamu la furaha badala ya kuamka na kutojikubali. Kama nilivyofundisha katika mada moja juu ya umuhimu wa kioo katika kujipa ujasiri na kutawala akili yako kwa kurudiarudia maneno na vitendo, basi unaweza kujitazama na kujikubali wakati siku ikianza. Halafu endeleza tabasamu hilo siku nzima na usiruhusu hali, kitu au mtu yoyote kukuharibia tabasamu hilo. 

Mitazamo ya watu haihusiani na uzuri.

Sio kila mtu anaweza kuuona uzuri wako, na sio kila mmoja anaweza kukuelewa kwa styles zako. Ni vigumu sana kutegemea kumfanya kila mtu aone kama wewe ni mzuri. Kwani macho na akili havifanani kwa wanadamu hivyo ni vyema kuweka akilini kuwa sio kila mtu anaweza kuona uzuri unaouona wewe. Wengi wamekuwa wakisikitika kuona wanahukumiwa kwa muonekano wao lakini ukiweka wazo hili akilini na kulielewa hautaweza kuumia kwa mawazo ya watu wanaokuona. 

Real beauty is to be true to oneself. That's what makes me feel good. - Laetitia Casta