Jifunze kutumia muda wako vyema
Posted by Apolinary Macha on 10:28 with No comments
Tumia muda wako vyema |
Kila mwanadamu anatofautiana katika jinsi na namna ambayo anatumia muda wake. kila mtu anatumia muda wake kwa namna tofauti, kwa maana ya kuwa unachofanya sasa kuna mtu anafanya tofauti. Kila wakati uliopo wanadamu mbalimbali wanafanya mambo tofauti tofauti na kupelekea kuwepo utofauti wa matumizi ya muda.
- Kuna mtu anatumia muda huu kupumzika
- Kuna mtu anatumia muda huu kulala
- Kuna mtu anatumia muda huu kusoma
- Kuna mtu anatumia muda huu kufanya majukumu yake ya kazini
- Kuna mtu anatumia muda huu kusoma mada hii
- Kuna mtu anatumia muda huu kuzungumza
Hivyo kila mmoja anatumia wakati uliopo kwa namna tofauti tofauti.
Usipothamini muda wako hakuna ambaye atauthamini
Tambua faida ya matumizi sahihi ya muda
Ukichunguza katika maisha, kinachotofautisha maisha ya wanadamu ni jinsi wanavyotumia muda wao. Katika kila wakati uliopo au muda uliopo, je unautumia kufanya jambo la maana katika kukusaidia au unafanya jambo ambalo sio la lazima sana. Katika kuishi kwa kutambua na kuwa makini na ufanyacho itakusaidia sana kuhakikisha unakuwa unautumia muda wako vyema. Kumbuka kuwa, ukitumia muda wako vyema itakusaidia hapo baadaye kuweza kutimiza malengo mengi na kuwa na mafanikio mengi kutokana na kutumia muda wako mwingi kuhakikisha unafanya maendeleo.Maisha ni mfupi na muda ni mchache sana
Kuna msemo unasema kuwa muda sio rafiki. Msemo huu unamaanisha kuwa, muda ni adui mkubwa wa maisha yetu. Tuna muda mchache sana katika maisha, kulinganisha na miaka mingi ambayo mwanadamu anaishi, ni miaka zaidi ya 100. Mwanadamu akiishi miaka 100 bado ni miaka michache sana ya kuishi. Kila wakati muda unasogea mbele na hakuna kurudi nyuma. hakuna nafasi ya kusema turudishe muda nyuma na kusahihisha jambo fulani. Pia hatuna uwezo wa kurudisha muda nyuma na ufurahia nyakati ambayo tunaikumbuka, kila nyakati inapita.Tumia muda wako sahihi
Muda ukishapita, ni umepita; katika hilo hatuna uwezo wa kurudisha muda nyuma wala kurekebisha matumizi mabaya ya muda. Ni vyema kila wakati tutafakari,JE NINAUTUMIAJE MUDA HUU ULIPO?
JE NINATUMIA MUDA HUU KWA MANUFAA AU NINAPOTEZA MUDA?
Ukiweza kujali muda wako utaweza kupanga malengo na kufikia malengo yako vyema bila matatizo.
0 maoni:
Chapisha Maoni