Kuwa Na Furaha
Posted by Apolinary Macha on 17:11 with No comments
Kuwa na furaha ni uamuzi wako, amua sasa.
Mtu akikuuliza je una furaha?
Ni swali gumu sana, kwani unaweza ukawa una furaha lakini unafahamu kuwa furaha hiyo haidumu milele. Labda una furaha kutokana na una familia nzuri, lakini kwa kina utaona kuwa furaha hiyo inategemea uwepo wa familia nzuri, na uwepo huo ukitenganishwa kwa vifo, maisha, mabadiliko mbalimbali basi furaha yake nayo inaisha. Hivyo kuna furaha za milele na furaha ya muda mfupi.
Kila mtu anapenda kuwa na furaha, na lengo kuu la maisha ni kuwa na furaha. Vifuatavyo ni moja kati ya vitu ambavyo vinaweza kukuongezea furaha ukivitambua.
Furaha haitoki nje yako.
Usijichoshe kuitafuta furaha kupitia vitu, mali, watu, hali, hisia, n.k bali furaha ipo ndani yako. Furaha inayopatikana nje ni furaha ya muda mfupi lakini ukijizoesha kupata furaha ndani yako utaiona furaha isiyo na kikomo wala hautakuwa na wasiwasi wa kupoteza furaha yako kwani inapatikana bure.Furaha haipatikani kwa kuwakosea wengine.
Katika kutafuta furaha yako hakikisha haumkosei mtu, hakikisha unaelewa kuwa na wanadamu wengine nao wanahitaji furaha. Ni furaha ukifahamu kuwa wanadamu wanaokuzunguka nao wana furaha, lakini furaha haiji kama unawakosea wengine.Furaha ni kama mwanga wa mshumaa, ukiwasha mishumaa mingine nao haupingui bali unaendelea kuwaka na kuisha taratibu kama mishumaa mingine, furaha haipungui kwa kushare furaha yako. - Buddha
Jifunze kuwaza mawazo chanya.
Pale unapoona mawazo mabaya yanakuja akilini kama vile chuki, wasiwasi, hasira, woga, kiburi, uongo n.k jitahidi kuvizuia hivyo vyote kwa upendo, furaha, amani, busara, shukrani, ukarimu n.k Kumbuka unaporuhusu mawazo mabaya ndipo unakaribisha hali mbaya. Akili inaumba kutokana na matendo, mawazo, na maneno.Kila la kheri katika kuitafuta furaha ya kweli. Asante.
Categories: Akili, Changamoto, Furaha, Happiness, Jitambue, Kujitambua, Maisha, Mawazo, Picha, Ufahamu
0 maoni:
Chapisha Maoni