Kwanini unapiga kelele ukiwa na Hasira?

Posted by Apolinary Macha on 15:20 with 2 comments

Kulikuwa na mwalimu mmoja wa kiimani alikuwa anaoga mtoni. Akakutana na wanafamilia wakigombana kwa hasira na kelele sana. Aliporudi kwa wanafunzi wake wa imani akawauliza,

"Kwanini watu wanapiga kelele wakiwa na hasira?"

Wanafunzi wake wakafikiria kwa mda, mmoja wao akasema "Kwa sababu mtu akiwa na hasira anausahau utulivu wa kiroho ndio maana anajikuta anapiga makelele na kutumia sauti kwa nguvu". 

Wanafunzi wengine wakajitahidi kutoa majibu yao lakini mwalimu wao hakuridhika na majibu kikamili ndipo akawaelezea kuwa:

"Pale watu wawili wanapokasirikiana, mioyo yao inakuwa mbali kwa kila mmoja. Na ili kuweza kurudisha umbali wa moyo wa mwingine ili uelewe unachotaka kuongea unajikuta unatumia sauti kwa nguvu sana kulipiza utofauti wa umbali wa roho pale unapotaka kusema kilichoko rohoni mwako wakati moyo wa mwenzio upo mbali. 

"Kwanini watu wawili wakipendana hawapigi kelele kuongea? Ni kwa sababu pale upendo unapokwepo roho zinakuwa karibu na kuunganika hivyo mmoja wapo anapotaka kujielezea (kuelezea kilichopo moyoni) anatumia sauti ndogo, taratibu kwani mioyo inakuwa karibu. 

"Hasira na chuki vinafanya mioyo kuwa mbali na maamuzi yanakuwa sio mazuri lakini upendo ukiwepo mioyo inakuwa karibu, inasikilizana na kuelewana". 

Akawatazama wanafunzi wake na kuwaambia, "Hivyo pale mnazungumza au kujielezea hakikisha moyo wako haupo mbali na wa mwenzio, epuka chuki, hasira, wivu au visasi bali tumia upendo kujielezea na amani moyoni."
Categories: