Usimtendee ubaya adui yako
Posted by Apolinary Macha on 14:09 with No comments
Usimtendee Ubaya Adui yako |
Katika maisha, hakuna mwanadamu asiye na maadui au watu wabaya, na hajawahi kutokea mwanadamu ambaye kila mtu anampenda. Ni kawaida katika maisha kuwepo kwa watu ambao wanakutakia mabaya na sio mema. Kila mwanadamu ana marafiki na watu wambao sio wema kwake, hivyo ni vyema kujua jinsi ya kuishi nao. Katika vitabu vyote vya dini tunahimizwa jambo moja kuu ambalo leo hii ningependa kutuma mtazamo huu ili kila mmoja ajue jinsi ya kuishi vyema na watu.
Msingi mkuu ni kuhakikisha hautendi mabaya kwa adui zako wala hauwatakii mabaya. Ukiwa na watu ambao wanakuombea mabaya wewe waombee mema, ukiwa na watu wanaokudharau, wewe waheshimu; Ukiwa na watu ambao wanakusema vibaya wewe waseme vizuri; ukiwa na watu wanaotaka kupigana, wewe usipigane bali eneza upenda.
Ni kwa sababu, kila unachotenda wewe utavuna wewe, na anachokutendea mtu atakivuna yeye. Mtu anayekutendea mabaya atapata mabaya; na ukimtendea wema utavuna wewe wema wako. Ni vyema kuwa makini na unachotenda wewe maana kuna mavuno yake kwako wewe, na anachokutendea mwenzako naye atavuna yeye (Sheria ya Karma).
0 maoni:
Chapisha Maoni