Sheria ya Kwanza: Sheria ya Chanzo na Matokeo (Cause and Effect).

Posted by Apolinary Macha on 10:32 with No comments


Inaendelea kutoka katika mada ya Sheria kuu kumi ambazo zinaongoza Ulimwengu. Hii ni sheria ya kwanza katika kuelewa sheria za ulimwengu wa ndani na nje yetu. Pia ni sheria ya akili na ufahamu. Endelea kufuatilia sheria zote 10 ambapo hii ni sheria ya kwanza na sheria 9 zilizobakia nazo zitafuatia.

Sheria Ya 1: Chanzo na Matokeo.



Mawazo yetu ndiyo yanayounda uhalisia wetu na sio vingine. Hii ni sheria ya kale sana tangu enzi za wanadamu wa kale waliopenda kuwa watafutaji wa ukweli wa ulimwengu walikutana nayo. Ni sheria ambayo inafahamika sana na imetafsiriwa katika maelezo tofauti tofauti katika imani tofauti tofauti.
Ni sheria Kuu.

Kama ilivyo leo, hakuna anayefahamu ni kwanini kuna sheria kama vile ya Gravity, sheria za sayansi, n.k. Na hata katika sheria hii hakuna anauejua kwanini sheria hii ipo lakini hiyo haijalishi, kinachopaswa kwetu sisi wanadamu ni kuielewa vyema na kujua jinsi inavyofanya kazi ili nasi tuweze kuishi nayo.

Wazo ndio chanzo, vingine vyote ni matokeo tu. 
Watu wengi hasa ambao hawajasoma sana wanafikiri kuwa vitu vya kifizikia ni halisi, wanafikiri ni kweli vitu hivyo vipo kifizikia. Kutokana na uelewa wao huo wanakuwa wanaamini sana ulimwengu wa nje yao na kusahau ulimwengu wa ndani yao. Huwezi kuelewa ulimwengu wa nje bila kuelewa ulimwengu wa ndani, ulimwengu wa nje ni matokeo ya ulimwengu wa ndani. Kutokana na kutoelewa huko watu wamekuwa wakiteseka na kuamini hawawezi kubadili maisha yao kwani hawajui chanzo cha maisha yao. Hawafahamu kuwa maisha yako ni matokeo ya uelewa wako wa ndani yako. 
Mfano mzuri katika kuelewesha hilo ni sawa na tunaangalia sinema, kumbe sinema hiyo inatokana na matukio yaliyopo ndani ya ufahamu wetu. Sio sinema iliyopo nje yetu bali chanzo chake cha matukio kinatokana na ufahamu wetu. Sinema yake ni kama display tu ya ufahamu wetu. Kutoelewa hayo wanadamu wengi wamekuwa watumwa na wanateseka kutokana na kutofahamu chanzo cha hayo yote ni nini. 


Kumbuka kuwa tunapoangalia sheria za kifizikia tunafahamu dhahiri kuwa HAKUNA JAMBO LISILO NA CHANZO. Na sheria hii ndipo iliposimamia. Hakuna jambo lisilo na chanzo na ndio maana inaitwa sheria ya chanzo na matokeo kwani kila tokeo lina chanzo chake. Hakuna matokeo yasiyo na chanzo kamwe.

Hivyo kama kila jambo lina chanzo chake, tunapaswa kufahamu kuwa uhalisia/reality ni illusion/Uongo kwani reality inatengenezwa na sisi wanadamu wenyewe na sio kwingine. Reality au uhalisia unaoishi unatokana na milango yako ya ufahamu, akili yako, imani yako na uelewa wako.

Kila kitu kina chanzo, huo ni uhalisia. Kila kitu kilianza kama ufahamu, mfano mzuri ni Computer, madirisha, nyumba, simu, nguo, sanaa, na vyote ambavyo vimetokana na ujuzi wa mwanadamu vilianza kama WAZO, baada ya kufanyiwa kazi vikatokea katika dunia ya kifizikia. Lakini hapo kabla vilikuwa ni Mawazo na sio physical things. 

Chunguza sana sheria hii, kila tokeo unaloliona lina chanzo chake, kufahamu sheria hii inakusaidia kuwa mtafutaji wa ukweli. Badala ya kupoteza nguvu katika matokeo unapaswa kufuatilia chanzo cha tokeo kwani kubadili chanzo ni kubadili matokeo. 

Walimu wakubwa wa ulimwengu huu wote wamefundisha sheria hii, wanaweza wakawa hawajakuambia moja kwa moja kutokana na kuwa uelewa wa wanadamu unatofautiana kwa jinsi wanavyoutumia lakini walimu hao wamekuwa wakitufundisha vyema kwa mifano. Mfano mzuri ni kuwa 
  • Unavuna unachopanda: Ukipanda maembe utalima maembe, ukipanda magugu utavuna magugu. Sheria hii ni sawa na kukuambia kuwa kila tokeo lina chanzo, kubadili chanzo ni kubadili matokeo. Huwezi kuvuna maembe katika tawi la mchungwa.
  • Sheria ya Karma: Ni sheria ya mashariki inayosema kuwa kila WAZO, TENDO na MANENO yana matokeo yake katika ulimwengu wako. Kutokana na hilo wakafundisha kuwa kuna Karma ya matendo, Kuna karma ya maneno na kuna karma ya mawazo. Hivyo kila tutendacho, tusemacho na tunachofikiria kina matokeo katika dunia yetu. Nimesema dunia yetu kwani kila mwanadamu anaishi katika dunia yake. Sheria hii nayo nitakuja kuieleza vyema.
  • What goes around comes around: Nayo ni sawa na kusema kuwa kunachokijia ni matokeo ya kilichotoka kwako. What comes around is the result of whats goes out of you. Unachokipata ni matokeo ya ulichokitoa.
Tutakapokuja kufahamu kuwa tunaishi katika ulimwengu unaoumbwa kutokana na ufahamu wetu, kwa kufahamu hayo ni hatua moja ya kwanza katika kuweza kubadili maisha yako na kuweza kuelewa kwanini wanadamu wengine nao wanaishi katika uhalisia tofauti na wewe. Kwa kuanza kuelewa hili utaweza kujiuliza mengi na kujikuta unafahamu chanzo cha mengi badala ya kupoteza muda katika matokeo. Wengi hupoteza muda kubadili matokeo kumbe matokeo ni matokeo, huwezi kuyabadili bali unaweza kubadili chanzo chake.

Maya Angelou aliwahi kusema sentensi moja nzuri sana -
Kama haupendi unachokiona kibadili, kama hauwezi kukibadili badili mtazamo wako.
Kwa kuweka sheria hii katika uelewa mzuri na kwa kufupisha vyema ni kusema kuwa:
Mawazo yetu yanaumba ulimwengu wetu, mawazo yetu ndio kiaishiria ya kinachofuatia. Kila jambo lina chanzo, chanzo kikuu na chanzo ambacho ndio cha mwanzo kabisa ni WAZO. Tunaishi katika dunia ambayo inatengenezwa na uelewa wetu. Ndio maana kila mwanadamu anaishi katika dunia yake kutokana na kuwa uelewa unatofautiana baina ya wanadamu. 

BADILI MAWAZO YAKO KUBADILI DUNIA YAKO.