Kwanini tunashauriwa kutenda mema?

Posted by Apolinary Macha on 14:42 with No comments

Tunatenda mema kwa sababu vitabu vya dini vinatushauri kutenda mema na kutusisitiza kuwa ukitenda mabaya kuna adhabu yake baada ya mwisho wa maisha ya hapa duniani. Ni kweli, huu ndio mtazamo ambao wengi wanaamini. Lakini pia kuna mtazamo mwingine unaosema tunatenda mema kwa sababu kuna manufaa kwetu, watu wanaotuzunguka, viumbe vinavyotuzunguka, ndugu, na mazingira; pia kwa manufaa yetu katika maisha haya haya ya hapa duniani.

Mtazamo wa pili ni mtazamo ambao ni wa muhimu sana kwa kila mmoja, kwa sababu kwanza mwanadamu anapaswa kufikiria kuhusu kuishi maisha haya kiusahihi kwanza. Maisha baada ya kifo hatuna uhakika nayo wala kiukweli hatujui yapoje lakini cha msingi ni kuweka uzito kwenye maisha ya sasa.

Kwenye maisha utagundua kuwa, kila mtu anayetenda mema anaishi kwa Amani bila taabu na wale wanaotenda Mabaya kuna taabu wanazipata. Mfano mtu anayelewa, mtu anayezini au mtu anayeiba, hawa wanapata taabu kuanzia katika maisha haya ya sasa na inaonekana katika maisha haya. Mfano kwa kupata magonjwa ya zinaa, magonjwa ya kutopendwa na watu, kupoteza mali, kutoendelea katika maisha n.k. 

Chunguza hili na utatambua kuwa kila tunalotenda linakaa kwenye makundi mawili, hasi na chanya. Kila upande una matokeo yake kuendana na upande huo. Ndio maana mtu anayejitolea kwa watu, mtu mnyenyekevu, mtu anayejituma, mtu anayefanya mazoezi, mtu anayekula vyakula sahihi, mtu anayesema ukweli, n.k. anaendelea na kuna mema anayapata hapa hapa duniani.

Kila tunalotenda linakaa kwenye makundi mawili, hasi na chanya. Kila upande una matokeo yake kuendana na upande huo. Ndio maana mtu anayejitolea kwa watu, mtu mnyenyekevu, mtu anayejituma, mtu anayefanya mazoezi, mtu anayekula vyakula sahihi, mtu anayesema ukweli, n.k. anaendelea na kuna mema anayapata hapa hapa duniani.

Kila jambo ambalo tunalitenda, tunaloliwaza na tunalolisema ni kama mbegu katika maisha yetu. Kila siku tunapanda mbegu mbalimbali katika matendo na mawazo yetu. Mbegu hizi kupelekea mazao ambayo ni sahihi kwetu au ambayo sio sahihi. Chukulia maisha ni kama vile bustani ambayo mwanadamu anapanda mbegu mbaimbali katika maisha yake na kila mbegu hukua na kuleta matokeo fulani.

Hivyo ni vyema sana tukazidi kujitambua na kuwa makini na matendo na mawazo yetu. Tuhakikishe kila mbegu tunayoipanda maishani kwetu ni mbegu sahihi na ambayo inakua na kuleta matokeo mazuri katika maisha yetu. Mbegu sahihi ni mawazo sahihi, matendo sahihi, fikra sahihi, jitihada sahihi, lugha sahihi na matendo yote ambayo ni sahihi katika maisha yetu.