Kwanini kukumbuka kuwa ipo siku utakufa inaweza kutufanya tuzidi kujituma na kuwa na amani

Posted by Apolinary Macha on 14:26 with No comments


Mojawapo kati ya quote mojawapo kuwa ya Steve Job katika kitabu chake ni pale aliposema kuwa, katika maisha yake siku aliyokuja kutambua kuwa kila mwanadamu atakufa ilizidi kumuhamasisha na kumpunguzia mawazo.

Ni jambo la kushangaza sana kuwaza kuwa ipo siku tutakufa. Kila mmoja wetu anapita kwenye hii dunia, tulizaliwa tukiwa hatuna chochote na tunafariki tukiwa hatuna chochote katika maisha yetu. Kifo kimekuwa ni sehemu ya kutisha sana katika maisha yetu, kila mwanadamu hapendi kutafakari kuwa ipo siku atakufa. Kutafakari huko tunaona kuwa kunapelekea tukate tamaa na kujisikia vibaya kuwa haya maisha tunayaacha. Sio kweli kuwa kuwaza hayo kunapelekea kweli tujisikie vibaya, kuna faida za kutafakari kifo katika maisha yetu. leo tungependa kujadili kidogo kuhusiana na mambo ambayo tunaweza kuyatafakari pale tunapowaza kuwa ipo siku tutakufa.


Ni kutuhamasisha kuwa maisha ni mafupi ni lazima tuyatume kiusahihi

Hii ni kweli, katika maisha kifo kinatukumbusha kuwa maisha ni mafupi saana kuliko tunavyotegemea. Kila tunapoamka na kuona tumepata nafasi nyingine ya kuishi tuwaze kuwa lazima tuyatumie maisha haya kiusahihi kabisa. Kila tunapokuwa tunatafakari kifo katika maisha yetu lazima tusiache kukumbuka kuwa tupo hai ili tuzidi kuendelea kujituma kufikia ndoto zetu na tutambue mwisho wa siku lazima tuwe tumefikia malengo.


Kila kitu kina mwisho, hata mateso na raha zina mwisho

Ni dhahiri kuwa kila mwanadamu alizaliwa bila chochote, hata nguo tulizaliwa hatuna. Mwanadamu na viumbe vyo huzaliwa bila chochote, bila mali, bila nguo, bila mali na bila pesa. Pia katika misiba tunaona kila mtu anayefariki anaacha kila kitu chake katika kaburi lake. Hakuna mwanadamu anayefariki na kuondoka na mali zake zote, kila kitu tunakiacha ikiwemo miili yetu nayo tunaiacha inakufa inaoza. Kutafakari haya tunaona dhahiri kuwa magonjwa yetu, shida zetu, taabu na vitu vinavyotuzunguka na hatuvipendi vyote tunaviacha. Sio tu vile vibaya, hata vizuri navyo tunavipoteza na mwisho wa siku hatuna cha kuringia na hakuna cha kusikitika.

Kumbukumbu hazifi

Kifo kinatukumbusha kuwa kila kitu kinapita lakini kumbukumbu zetu juu ya vitu, watu au matukio vinabaki akilini mwetu daima na hivyo tujifunze kutengeneza kumbukumbu sahihi katika maisha yetu bila kuwatumia watu au vitu vibaya.

Kuacha kila kitu ambacho kilikuwa ni kigumu kuacha

Katika maisha yetu, kila mwanadamu kuna ambayo anatamani yasingekuwepo kwenye maisha yetu lakini hatuwezi kuachana navyo kwa sababu tayari tumeshashikiliwa. Inawezekana kuwa ni mazoea, watu, vitu, mali, n.k ambavyo tunatamani tungeviacha. Kuwaza kuwa ipo siku tutakufa inaweza kuwa ni njia mojawapo

Ni kutukumbusha kuwa hakuna kinachobaki milele

Kauli hii ya hakuna kinachobaki milele imekuwa ikitumika sana katika kutukumbusha tusijishikilie na chochote kile ambacho tunafikiri kitakaa milele. Sio mateso, raha, mali au chochote kile kinachobaki milele. hata jengo ambalo limejengwa, huchakaa, huzeeka na kuvunjwa ili lingine lijengwe.

Utagundua kuwa maisha ni zawadi kubwa sana

katika kila kitu kwenye maisha yetu, ni kutokana na kuwa tuna uhai. Ni kupitia uhai na kuishi kwetu ndio tunakutana na watu mbalimbali, ndugu, marafiki, mali n.k. Kama tusingekuwa hai tusingeweza kufanya haya yote ambayo tunayafanya hivi sasa. Hivyo tunategemea kabisa kuwa katika kutafakari kuwa ipo siku tutafariki, inatufunza kutambua kuwa haya maisha ni mafupi na bahati sana kuyaishi. Hivyo tuishi kwa kushukuru kila jambo hasa kwa uhai wetu na uwepo wetu kwenye huu ulimwengu.

Kila siku tunapoamka tutafakari kuwa tutakufa, hivyo tuyatumie maisha haya kiusahihi.