Tenga muda wa kutafakari.

Posted by Unknown on 18:03 with 1 comment
Tenga muda wa kutafakari.


Panga ratiba ya kutumia dakika chache angalau 10 ambazo utazitumia katika kutafakati maisha yako. Unaweza ukatumia wakati huo hata kwa kusoma kitabu cha msingi kitakachoweza kukusaidia katika maisha yako. Unaweza ukapanga pia wakati huo kabla ya kulala.

Unaweza kutumia wakati huo kufanya meditation, kuitafakari siku yako, au kusikiliza motivational audio (mafunzo ya kwenye sauti kwa simu). Kama wewe tayari unafahamu jinsi ya kufanya meditation vyema pia unaweza kutenga hata dakika 10 kila asubuhi uamkapo kabla ya kufanya chochote au kabla ya kutoka kitandani. Fanya meditation ya kujifunza kuitazama akili yako na fikra zako zilivyo na pia unaweza kumalizia kwa sala huku ukishukuru kwa kila jambo katika maisha yako.

Unaweza ukatenga muda pia wa kusoma kitabu ambacho ni cha umuhimu. Kinaweza kikawa ni kitabu cha imani, kitabu cha mafanikio au cha kufundisha maisha, kitabu cha maneno na mafundisho ya mtu anayekuhamasisha. Inaweza ikawa ni makala kwenye mtandao au pia inaweza ikawa ni website ambayo unapenda kutembelea kwa lengo la kujifunza mengi.

Tumia pia wakati wa kujitafakari. Jitazame, panga malengo yako ya siku katika wakati huo unaoutenga. Weka muda utakao kuwa unatenga kwa mambo hayo na kisha ufuate muda huo ipasavyo. Itakusaidia sana hapo baadae.