Elimu na Maarifa katika kuishi kwa amani, salama na kuwa upendo ni muhimu sana katika Maisha Yetu

Posted by Apolinary Macha on 16:05 with 1 comment

Kuwa mjinga ni hasara, ni kwa sababu kuwa mjinga kunapelekea madhara katika maisha yetu na kutufanya tusiishi vyema. Tangu enzi na enzi, vitabu vingi duniani vimekuwa vikijaribu kutufundisha kuwa hekima, elimu na maarifa ni vitu vya pekee sana kwa mwanadamu. Ni katika kutulinda na kutupatia elimu ambayo itasaidia kizazi hadi kizazi, wanadamu na Jamii zote.

Kuwa mjinga na kutotambua njia sahihi ya kuishi katika maisha na kukabiliana na changamoto mbalimbali ni kosa na inaweza kuwa ni dalili za kushindwa kuyatumia maisha yako kiusahihi. Wahenga walisema, Bora mjinga anayetambua yeye ni mjinga kuliko yule ambaye hatambui kabisa kuwa ni mjinga.

Msemo huu unatuonyesha hatua ya kwanza ya mwanadamu kuanza kujitambua na kuitafuta elimu ni pale anapokiri na kutambua kuwa yeye ni mjinga. Ni hatua ya kwanza inayozalisha hatua ya pili ya kuweka nia na juhudi za kuondoa ujinga.


Zipo njia mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzifuata katika kuujua ukweli na kuongeza ufahamu na utambuzi:-
• Dini mbalimbali
• Elimu ya Shule
• Wazazi/Walezi
• Wanafalsafa mbalimbali walioacha hekima
 • Mtandaoni
• Vitambu mbalimbali etc

 Katika kujifunza na kuongeza maarifa, ni vyema sana kuwa na akili ambayo ina uhuru wa kujifunza. Kuna falsafa, dini na walimu Wengi duniani. Ambapo ni vigumu kujua kila falsafa na elimu. Hivyo ni vyema sana kuhakikisha tunachukua kile ambacho kina uhalisia, manufaa na kinachotusaidia kuishi vyema katika maisha haya. Pia uhuru wa dini ni muhimu katika kuchambua mambo mengi na kupata utambuzi. Tukumbuke kuwa dini nyingi ni falsafa ambazo zilikuzwa na Jamii fulani katika utambuzi wao, ziliathiriwa na historia na matukio mbalimbali.

Ni vyema kujifunza kila dini na kuwa na uhuru wa kuchambua mambo na kuchukua yale yenye manufaa kwako na mwanadamu mwenzako. Elimu na maarifa katika kuishi kwa amani, salama na kuwa upendo ni muhimu sana. Ni muhimu kila siku tukijifunza, tukijichunguza na kupata muda wa kutafakari na kuyatazama maisha kama shule ya kujifunza ili kukua na kujitambua zaidi.


Asante