Mwaka 2018 unakaribia kuisha, kwani zimebaki wiki chache mwaka kuisha na kuingia mwaka mpya wa 2018. Kwa mtu mwenye busara atajiuliza sana maswali mbalimbali ya msingi kuhusiana na mwaka huu.
Maswali ya Msingi ya Kujiuliza:
- Je nini/kipi ambacho hutasahau mwaka 2018?
- Je mwaka 2018 umeutumia vyema?
- Je mwaka 2018 umeutumia kivipi katika kuboresha maisha yako na kupanga malengo yako?
- Je ni vipi unavyopaswa kubadili au kuboresha katika mwaka unaokuja?
Ni jambo la busara sana kutafakari. Lakini msingi mkuu ni kuhakikisha kuwa; katika matendo yako, maneno yako, na katika tafakari zako unapaswa kuzibadilisha kwa kuhakikisha unazidi kuendeleza hali hizo tatu na kuziboresha. Ukiweza kuboresha mawazo yako, matendo yako na maneno yako kiusahihi utaweza kubadili maisha yako vyema. Hivyo kaa na tafakari, mwaka 2018 umeutumia kivipi. Ikiwezekana andika hata katika kitabu chako au diary ya kumbukumbu itakusaidia kuhakikisha unapanga malengo mazuri na unatambua maendeleo yako ya kimaisha.
Brother shukran sana ubarikiwe umenifungua kwa mengi
JibuFuta