Sababu 6 za kutafakati katika kuendelea kusonga mbele na kutokata tamaa.

Posted by Apolinary Macha on 19:05 with 1 comment

Usiache kusonga Mbele, 
Usiwe na Mashaka juu ya mwendo wako kuwa taratibu au changamoto unazopata. Cha msingi ni kuendelea kusonga Mbele, haijalishi ni taratibu au kwa haraka


Sababu 6 za kutafakati katika kuendelea kusonga mbele na kutokata tamaa.
  1. Usikate tamaa; kabla ya kukata tamaa kwanza jiulize ni kwanini ukate tamaa. Unapokata tamaa hutaendelea kujaribu bahati yako na jitihada zote ambazo umefikia zifikirie unaenda kuziacha na kukubali kushindwa.
  2. Hata kwenda mbele taratibu ni hatua. Unaweza kukata tamaa kutokana na kuwa unahisi mwendo wako ni taratibu na ungetamani ungeenda mbele kwa haraka zaidi. Kumbuka kuwa hata hatua za taratibu ni mwendo, cha msingi haujasimama sehemu moja na unaendelea kusonga mbele.
  3. Kumbuka kuwa maisha sio mashindano. Usikubali kujilinganisha na mwendo wa wengine katika maisha na kutimiza malengo. Kila mwanadamu ana hatma yake na wewe weka umakini kwenye nia yako na jitazame mwenyewe, epuka kujilinganisha na watu wengine. 
  4. Kuwa na mtazamo chanya (Positive thinking). Kabla ya kukata tamaa tazama machache uliyoweza kuyafanikisha katika mipango yako na weka mtazamo wa kushukuru kwa ulipofikia na kwa kujipongeza hata kwa madogo ambayo umeyafikia. Jifunze kushukuru hata mambo madogo ambayo umeyafikia na usijione hujafanya chochote mpaka ulipofikia. 
  5. Jifunze kupumzika na kuruhusu muda kufanya kazi yake. Sio kila saa lazima ujipe mawazo na wasiwasi, kuna muda unatakiwa kupumzika na kutuliza akili kidogo kabla hujakata tamaa au kuhisi kuwa hausogei mbele katika malengo yako. Sio kila muda unatakiwa uwaze sana, ukiona jambo unaliwaza sana jipe hata muda mfupi wa kupumzika kutafakari kisha utarudi kuendelea kutafuta hatma yake kabla ya kukata tamaa. 
  6. Jifunze kukua na changamoto. Unapokata tamaa inamaanisha umekubali changamoto zikushinde na hutoendelea mbele. Kwanini ukubali changamoto zikushinde? Changamoto zipo kwa ajili ya kutukuza kifikra na kujifunza mengi katika maisha yetu. Usitazame changamoto kwa moyo mwepesi, weka msisitizo kushinda changamoto zako na endelea kupambana kuhakikisha unazishinda.

Kabla ya kukata tamaa tafakari haya!!!