Mbinu Kuu 5 za Kuhakikisha Unakabili Changamoto Vyema

Posted by Apolinary Macha on 11:20 with No comments



Katika maisha yetu, kila mmoja anakutana na changamoto mbalimbali kwenye jamii na kwenye majukumu yetu. Ni wazi kuwa, changamoto ni hali ya kawaida kabisa kwenye maisha. Zipo changamoto mbalimbali kama vile magonjwa, mifarakano, ajali, kukosa ajira, kutalikiana, upweke, na vifo au changamoto mbalimbali ambazo kwa katika kila namna kuna watu wanakutana nazo kwenye maisha. Leo katika mada hii tutajaribu kuangalia mbinu ambazo unaweza kuzitumia katika kupunguza msongo wa mawazo au kukosa furaha katika changamoto ambazo zinawakumba wanadamu. 

1. Kukubaliana na uhalisia

Kuna baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kukufanya ukatae uhalisia na kutokubaliana na hali. Changamoto hizi ni zile ambazo mwanadamu anakataa kukubaliana na hali. Mfano kupoteza mweza, kutalikiana au kuachana na mweza wako, ajali, magonjwa au kifo. Hizi changamoto zinapotokea, wanadamu wengi wanapenda kukataa uhalisia. Na jinsi unavyobisha inaweza kuongeza mawazo na kukosa amani, lakini ungekubali uhalisia kuwa ndio huo, ungeweza kuwa na furaha kwenye maisha. Wengine wanapofikia hatua hii husema "Ninakabidhi yote kwa Mungu", huu ni msemo wa kumaanisha unakubaliana na hali. 

Pia kuna changamoto nyingine zinatokana na kukataa ukweli na kupelekea mtu kutotafuta suluhisho. Njia ya kwanza katika kusuluhisha changamoto nyingi ni kutambua ukweli na kukubali uhalisia, baada ya hatua hiyo utaweza kufanya maamuzi ya kujua suluhisho maana utakuwa umeshakubaliana na hali. 

2. Jifunze kufurahia wakati uliopo na kuridhika na hali. 

Mojawapo kati ya kitu kinachokosesha furaha kwa watu wengi, wanaamini kuwa furaha inapatikana pale ambapo una kitu unachokitaka. Sio kweli, kwa sababu furaha unaweza kuipata wakati wowote na hata kwenye shida. Unaweza kuamua kuwa na furaha sasa hivi bila kujalisha upo kwenye hali gani. Ukiwa kwenye changamoto, unaweza kuvuta pumzi na kuacha akili isishikiliwe na mawazo na hisia za huzuni. Furahia una pumzi, toka nje tazama jua na mazingira mazuri kama vile maua mazuri, mito, wanyama wazuri ili uwe umepata dakika chache za kusahau mawazo. 

3. Jifunze kushukuru

Wanadamu wengi wanapokwepo kwenye changamoto za maisha wanapenda kusahau kushukuru. Si kweli kuwa kuna mwanadamu mwenye shida tu. Katika maisha hakuna shida tu, pia lazima kuna baraka na vitu vya kushukuru. Jifunze kushukuru kwa kile ambacho unacho kwa sasa na kwa hali nzuri ya maisha ambayo unayo. Shukuru kwa kila jambo na acha KULALAMIKA


4. Jifunze Kuchukulia Kawaida Maumivu

Kama ilivyosemwa hapo awali kwenye hatua ya kwanza, ni vyema kujifunza kukubaliana na hali na kuzoea hali zote nzuri na mbaya. Ukiweza kuwa na utaratibu huu utaweza kabisa kuwa na ujasiri wa kukutana na changamoto zote na hali zote ambazo hupendi. Ni kutambua kuwa kwenye maisha kuna chanya na hasi, na kila mwanadamu anatakiwa kujifunza kuvikabili vyote. 


5. Fikiria kwenye suluhisho

Jifunze kuwa mwepesi katika kuwaza kwenye njia za kusuluhisha na sio kutazama matatizo tu. Ukiwa na mazoea haya utaweza kupunguza changamoto kwa sababu utakuwa utakuwa unawaza mambo mengi ya kukusaidia na changamoto zako utakuwa unazipunguza. Hii ni kwa wale ambao wanawaza shida tu bila kuwaza suluhisho. Weka fikra kwenye 70% kuwaza suluhisho na 30% kuwaza changamoto kwa maana ya kuwa unaweza akili yako kwenye kutatua matatizo na changamoto badala ya kuwaza kwenye matatizo tu.