Maana Ya Ufahamu.
Posted by Apolinary Macha on 17:34 with No comments
Ufahamu kwa lugha ya kingereza ni consciousness.
Ufahamu wako ndio tofauti iliyopo kati yako na beings au wanadamu wengine kwa sababu ndio tofauti ilipo.
Wanadamu wanatofautiana ufahamu kwani ufahamu ni uelewa, maarifa, busara, kumbukumbu tulizo nazo akilini n.k katika safari tofauti za maisha. Mwanadamu anapozaliwa au anapoingia duniani katika hali ya kifizikia au katika hali ya kuwa na mwili na kuiona dunia tangu akiwa mdogo anajifunza mambo mbalimbali kama vile lugha, sheria za jamii inayomzunguka, kumbukumbu ndogo ndogo, busara, n.k vyote hivi anajifunza kupitia milango yake ya ufahamu kama vile macho kwa vitu vya kutazama, ulimi kwa kuonja, ngozi kwa kugusa, masikio kwa kusikia na pua kunusa, vyote hivi vinasababisha uumbaji wa "reality" yako au maisha yako. Mfano leo hii unaweza ukawa na imani fulani au dhana fulani kichwani ambayo unaiamini lakini unaweza usijue ni nini kimepelekea wewe kuwa na imani hiyo.
Mfano unaweza ukawa unaamini watu wa aina fulani ni wabaya au wakatili, lakini usijue ni kwanini unaamini hivyo. Unaweza kujichunguza kwa dhani na kutambua ni kutokana na tukio fulani ambalo lilikukuta au uliona kwa mwenzio na likakutengenezea dhana ya kuamini vibaya. Hivyo kila siku unaboresha ufahamu wako kwa kujifunza, kwa kutumia milango ya fahamu n.k.
Categories: Ufahamu
0 maoni:
Chapisha Maoni