Fahamu Haya Unapotaka Kufanya Mabadiliko Yoyote
Posted by Apolinary Macha on 20:09 with No comments
Kuna wakati kila mmoja anapenda kufanya mabadiliko fulani. Inaweza ikawa ni hali unapenda kuibadili, kitu, au chochote kila. Hamu ya kufanya mabadiliko mara nyingi inaanza pale unapokuwa hupendi hali iliyopo au kilichopo ndipo unapata hamu ya kufanya mabadiliko.
Tambua Kiini Cha Matokeo
Kabla ya kufanya mabadiliko yoyote tambua mzizi mkuu wa matokeo au hali unayoiona. Kila jambo, kila kitu, na kila hali ina chanzo chake. Chanzo chake ndicho kinachopelekea uwepo au matokeo yake. Kama hujakitambua chanzo ni vigumu sana kufanya mabadiliko. Huwezi kufanya mabadiliko katika kitu ambacho hufahamu chanzo chake. Ni sawa na kutaka kubadili aina ya maji yapitayo katika mto bila kufahamu chanzo cha maji hayo. Utakapoweza kubadili chanzo cha maji yalipotokea ndipo utaweza kubadili maji yake. Huwezi kubadili muembe kutoa machungwa bila kutambua chanzo cha maembe ni mti wa maembe.
Mfano wa Ua.
Unapotaka kubadili Ua, au kama unapenda Ua lichanue vyema, utahakikisha unaandaa mazingira mazuri, utalipa maji ya kutosha, utalipa rutuba ya kutosha na kuliepusha na mazingira ambayo yatalisumbua kukua vyema. Huwezi kulilazimisha Ua kuchanua kwa lazima. Lakini ukitaka Ua lichanue vyema litengenezee mazingira mazuri ambayo yatalipa vinavyohitajika kisha litachanua lenyewe vyema.
Kutambua kiini cha mabadiliko yoyote, ni fursa nzuri kuweza kubadili hali. Kaa tafakari, nini cha muhimu katika mabadiliko yoyote ya kwako ya maisha na kisha jitahidi kukibadili taratibu kwa kutambua kiini na kitumie vyema.
Tambua Kiini Cha Matokeo
Kabla ya kufanya mabadiliko yoyote tambua mzizi mkuu wa matokeo au hali unayoiona. Kila jambo, kila kitu, na kila hali ina chanzo chake. Chanzo chake ndicho kinachopelekea uwepo au matokeo yake. Kama hujakitambua chanzo ni vigumu sana kufanya mabadiliko. Huwezi kufanya mabadiliko katika kitu ambacho hufahamu chanzo chake. Ni sawa na kutaka kubadili aina ya maji yapitayo katika mto bila kufahamu chanzo cha maji hayo. Utakapoweza kubadili chanzo cha maji yalipotokea ndipo utaweza kubadili maji yake. Huwezi kubadili muembe kutoa machungwa bila kutambua chanzo cha maembe ni mti wa maembe.
Mfano wa Ua.
Unapotaka kubadili Ua, au kama unapenda Ua lichanue vyema, utahakikisha unaandaa mazingira mazuri, utalipa maji ya kutosha, utalipa rutuba ya kutosha na kuliepusha na mazingira ambayo yatalisumbua kukua vyema. Huwezi kulilazimisha Ua kuchanua kwa lazima. Lakini ukitaka Ua lichanue vyema litengenezee mazingira mazuri ambayo yatalipa vinavyohitajika kisha litachanua lenyewe vyema.
Unapotaka kubadili jambo, tambua kiini chake kisha kibadilishe. Tambua
chanzo cha mabadiliko kisha utaweza kubadili mabadiliko yake.
Ukiweza kubadili CHANZO, utaweza kubadili MATOKEO YAKE.
0 maoni:
Chapisha Maoni