Jinsi ya Kuifanya Siku Yako iwe Vyema

Posted by Apolinary Macha on 12:09 with 1 comment

  • Amka mapema: sali, tazama jua linavyochomoza, fanya meditation (taamuli), mazoezi, na panga siku yako.

  • Pangilia mipango na weka kipaumbele: Fahamu vitu vaya muhimu vya kufanya katika siku yako, panga muda wako.

  • Soma kitabu hata kimoja katika siku yako

  • Kula chakula chako taratibu, usile chakula kwa haraka, weka umakini kwenye chakula, furahia ladha ya chakula, usile ukiwa unafanya mambo mengi kama vile kuchezea sikmu au kuongea sana.

  • Tafuta muda wa kutembea, tazama mazingira, tazama uoto wa asili, sikiliza sauti za ndege, tazama bahari, na tumia muda kuwa peke yako ukiwa unatafakari na kufurahia ukimya kwa asubuhi au jioni.

  • Tumia muda kidogo kutazama kitu chochote ambacho kitakufanya ufurahi. Tazama kipindi cha television au video ambayo itakufanya ucheke na kufurahi. Sio lazima utazame kwa muda mrefu, bali unaweza kutenga dakika chache tu.

  • Katika siku yako hakikisha unatumia muda kufanya kitu ambacho unapenda. Piga gitaa, andika, cheza mchezo uupendao, imba au fanya chochote unachopendelea.

  • Fanya jambo moja kwa wakati, epuka kufanya mambo mengi wa wakati mmoja.

  • Saidia wenzako, kila siku hakikisha unajitahidi kufanya jambo lolote ambalo litamfanya mwanadamu mwenzako awe na furaha.