Weka NIA na ULAZIMA Katika Mambo Ya Muhimu Kwenye Maisha
Posted by Apolinary Macha on 16:17 with 1 comment
Weka NIA na ULAZIMA Katika Mambo Ya Muhimu Kwenye Maisha
Ni mara ngapi umekuwa ukijiambia mwenyewe
“Natakiwa kufanya hivi…Ninatakiwa kuwa na kazi…Ninatakiwa kuanzisha mtaji...Natakiwa kusoma kwa bidii…Natakiwa kuwa na urafiki mzuri na familia yangu…Natakiwa Kuacha pombe…Natakiwa kuacha kuvuta sigara…”
Watu wengi wana orodha ya vitu na mambo mbalimbali ambayo wanapaswa kutimiza. Orodha hiyo ikikamilika itapelekea manufaa fulani katika maisha. Wengine wamekuwa wakiweka “Years resolution” kuhakikisha kuwa kila mwaka wanatimiza malengo fulani na kufika pale wanapolenga. Kufanikisha malengo hupelekea kupata furaha na amani na kushindwa kufanikisha malengo hupelekea mtu kujisikia vibaya kutokana na kufeli na kukata tamaa.
Lakini Je inawezekana kubadilisha unachopaswa kufanya kiwe LAZIMA? Ikiwa na maana kuwa badala ya kusema ‘Unapaswa kufanya ….’ unasema NI LAZIMA KUFANYA ….’ Kujaribu njia hiyo inapelekea urahisi wa mtu kubadili maisha yake na kujituma kutimiza yale ambayo anapaswa kufanya. Haitakuwa kwa kujisemea tu bali inakwepo kwa kuamua kwa dhahiri na kwa kujiwekea nadhiri ya kutimiza badala ya kuamua bila nadhiri kamili.
Kama kweli umeweka nia ya kubadilika au kufikia lengo fulani, ni vyema kuweka nadhiri na adabu katika nia hiyo.
Chukulia mfano wa mtu ambaye anasema “Ninataka niache kuwa mlevi, lakini ulevi ni kitendo ambacho nimejizoesha, siwezi kuacha ulevi”.
Kauli hiyo hupelekea Akilini mtu kuona haiwezekani kuacha, na hujikuta inakuwa ni vugumu kuacha.
Asilimia kubwa sana ya watu wanavyoishi hivi sasa umeadhiriwa na jinsi walivyokuwa wanajichukulia, mazoea yao na jitihada zao miaka 10, 20 au 30 iliyopita. Tangu ulipokuwa mdogo kuna mambo mambo mbalimbali ambayo umekuwa ukiamini, kujizoesha na kujichukulia. Imeweka adhari kubwa mpaka sasa na katika maisha ya sasa, inawezekana ukafahamu hilo au ukashindwa kufahamu ni jinsi gani imeweka madhara fulani katika maisha yako.
Unajichukuliaje?
Lini uliacha kujitazama kihivyo?
Umeridhika na jinsi unavyojielewa?
Kuna haja ya kujiboresha na kufika mbali na ulipo hivi sasa?
Kipi unachopaswa kufanya hivi sasa?
Wengi hufikia hatua ya juu kabisa kwa kuamua kutoka katika vifungo vya mazoea na mashikilio ya maendeleo yao na kuanza kuweka jitihada taratibu taratibu.
Jinsi unavyojichukulia na unachopaswa kufanya ni mambo ya muhimu kuyatambua na kuweka nia ya ULAZIMA. Ni vyema kuacha visingizio na kuweka jitihada yoyote unayopaswa kufanya.
The strongest force in the human personality is the need to stay consistent with how we define ourselves. And you may just find that by making these changes, you can make lasting change in your quality of life.
Categories: Badilika, Changamoto, Jitambue, Maisha, Malengo, Mambo ya Muhimu, Mipango, Ndoto na Malengo, Ujumbe
True indeed
JibuFuta