Vifungo Ambavyo Jamii Inakufunga.
Posted by Unknown on 17:08 with No comments
Kifungo cha Akili ambacho Jamii inatufunga. |
Kifungoni ni wapi? Je ni kama mahabusu? Hapana, nikisema kifungo ninakuwa ninamaanisha pale ambapo panakunyima uhuru au unapokosa nafasi ya kuwa wewe kama wewe. Pulizo ni kama vile kifungo cha kidunia ambacho kila mmoja wetu anakuwa ndani yake. Mfano kifungo hicho kinaweza kuwa ni
- Wasiwasi wa wakati ujao,
- Dhana unayoifahamu juu ya mafanikio katika maisha,
- Kulazimisha kupendwa na kila mtu,
- Kulazimisha kumfurahisha kila mtu,
- Kulazimisha kuwa mkamilifu,
- Maneno ya watu,
- au Imani ambayo hauna uhuru au uhakika nayo.
- Jinsi ya kuishi,
- Jinsi ya kuvaa,
- Jinsi ya kula,
- Kipi cha kula na kipi cha kutupa,
- Dini/Imani gani ipo sahihi,
- Wewe ni nani na kwanini upo hapa,
- Miziki, Television na vyombo vingine vya habari visemavyo,
- Matangazo yakikuambia kipi cha kununua au cha muhimu na bora kuliko vingine,
- Maana ya mafanikio ni nini,
- Kazi gani ni ya maana kuliko nyingine na mengi ambayo jamii imeona ni mazuri kwao basi nao hupenda yawe mazuri kwako.
Jamii inatuweka kwenye pulizo, hivyo ni vyema kutoka nje ya pulizo ili kuufahamu ukweli. Ukweli hauwezi kuufahamu kwa kuambiwa tu bali nawe unapaswa uuthibitishe. Je aliyeanzisha ukweli huo aliambiwa na nani? Kwanini na wewe usiutafute? Kwa kuacha kulazimisha mambo unaweza ukajikuta unajifunza mengi sana kuhusiana na maisha kwa ujumla, na ikakusaidia kutafuta dhumuni lako la maisha.
Weka Huru Akili Yako |
Kama unatafuta dhumuni lako la maisha kwa kutegemea jamii ikuchagulie dhumuni la kuishi utamaliza maisha yako hujaishi maisha yako bali unaishi maisha ya wenzako. Ili kuijua safari yako ina malengo gani toka nje ya pulizo na chunguza ndani mwako unapenda nini na jamii inakuambia nini. Mfano kuna anayependa kuwa daktari lakini wazazi wanamwambia awe fulani. Sio kwamba wazazi wamekosea, nao wapo sahihi. Jitahidi uwaelewe kwani kuna wakati mtu hukuchagulia maamuzi kwa kukulinda na kwa kutumia akili aliyonayo yeye, hivyo nawe unapaswa kutambua ni kwanini mtu anakupa mtazamo fulani na kisha amua mtazamo wako kiusahihi na bila kubishana au kumdharau mtu. Heshimu kila mtu na tambua mchango wa kila mtu katika maisha yako.
Kifungo cha Akili |
0 maoni:
Chapisha Maoni