Sheria Kuu Kumi za Hali ya Akili ya Mwanadamu (Mental Laws)
Posted by Apolinary Macha on 17:35 with No comments
Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.
SHERIA HIZO NI:
- Sheria ya Chanzo na Matokeo
- Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
- Sheria ya Umakini/focus
- Sheria ya Mawazo
- Sheria ya Ubinafsi
- Sheria ya Uumbaji
- Sheria ya Hisia
- Sheria ya Ubadili
- Sheria ya Usawa wa Akili
- Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?
Mapinduzi makuu ya sasa ni ufuatiliaji wa asili na jinsi
akili ya mwanadamu ilivyo. Sayansi ya kufuatilia akili ya mwanadamu ilivyo ni
sayansi ambayo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa kwani akili ya mwanadamu
ina sayansi kubwa sana. Asilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu inatengenezwa na
akili yake hivyo katika elimu hiyo utaweza kufahamu mengi sana kuhusiana na
mwanadamu na jinsi akili yake inavyofanya kazi vyema.
Mlolongo huu wa mada utakuwa na mada kumi, ambapo kila mada
itaelezea sharia yake kwa undani kwani kuweka mada moja kuelekeza mad azote hizi
kutapelekea uchache wa maelekezo.
Sheria
Kwa lugha nyingine huita “Laws”. Sheria ni kama maelekezo ya
suala au jambo Fulani. Wengi wanafahamu sharia ya mvutano, ni sheria inayosema
kuwa ukirusha kitu juu basi huvutwa kwenda chini kuelekea ardhini. Ni sheria
ambayo uwe unaijua au usiijue ukijirusha gorofani lazima uanguke chini. Sheria
kuwepo haimaanishi mpaka uijue ndipo matokeo yake huonekana bali hata ukiwa
haujui bado sheria itafanya kazi yake katika mangilio wake unavyotaka.
Zipo sheria mbalimbali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikilinda
taratibu nyingi. Je umewahi kujiuliza kama kuna sheria au taratibu Fulani ambazo
ukizielewa utaweza kufahamu jinsi akili inavyofanya kazi? Ni sawa na mkulima,
akipanda maembe atavuna maembe, hata kama anajua kuwa anavuna anachopanda au
hajui kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya anachovuna na anachopanda bado
atapata matokeo sawa. Hivyo ni vyema kufahamu sheria hizo. Ni vyema kufahamu
kwani itakusaidia kuweza kuongoza matokeo. Ukiwa unajua kuwa taratibu Fulani hupelekea
matokeo Fulani inakusaidia kutengeneza wakati ujao katika njia njema na kupata
matokeo mazuri.
Mfano wa sheria nyingine ni sheria za rangi, kila mmoja
anafahamu ukichanganya nyekundu na njano unapata machungwa, ni sheria kwani
lazima itokee hivyo. Uwe unajua hilo wakati unachanganya au haujui lakini
lazima matokeo yake yatokee. Ukichanganya blu na yellow utapata kijani, hiyo ni
lazima. Labda uwe haujachanganya vyema au tatizo linguine lakini
zikishachanganyika matokeo yake ni mengine.
Sheria zilikwepo tangu mwanzo wa ulimwengu na zitazidi
kuwepo. Huenda kuna sheria nyingi ambazo bado hatujazijua kutokana na uelewa
wetu lakini haimaanishi hazipo, bado zipo tu. Galileo Galilei alipofahamu kuwa
kuna Gravity na kuelezea sheria ya kuvutwa vitu chini haimaanishi kabla yay eye
kuelezea ilikuwa haipo. Bali alichofanya yeye ni kuifahamu sheria na sio
kuianzisha sheria. Unaweza ukatumia sheria kwa mafanikio. Mfano kutokana na
uelewa kuwa kuna kani ya mvutano wa tumetengeneza meli (kwa kuhakikisha
haizami), tumetengeneza ndoo na vyomba vya kuhifadhi maji kwa kuziba chini, n.k
vyote hivi ni kutusaidia kuweza kuishi katika cheria tulizozikuta.
SHERIA KUU ZA AKILI YA MWANADAMU.
Kama dunia ilivyo na sheria zake, serikali zilivyo na sheria
zake, dini zilivyo na sheria zake, tamaduni Fulani za watu zilivyo na sheria
zako fahamu kuwa hata akili nayo ina sheria zake. Kuna sheria za biolojia, jeographia,
fizikia, n ahata saikolojia. Fahamu kuwa n ahata akili ina sheria zake. Sheria
hizo hutawala maisha ya mwanadamu kwani kila mwanadamu ana akili yake lakini
akili zote zina asili moja na sheria moja, tofauti ni utumiaji.
Fahamu kuwa unaweza kuiongoza akili yako na kuitawala akili
yako. Akili ni chombo kizuri sana kwa kubadilika lakini pia ni chombo kibaya
sana kwa kupotoka.
Mada za Kuhusiana na Sheria hizo zinafuta, na kila sheria itaelezewa katika mada yake na mifano hai ambayo itakufunua mwangaza na kuelewa vyema jinsi akili ya mwanadamu ilivyo ya ajabu.
Endelea kufuatilia...
Categories: Jitambue
0 maoni:
Chapisha Maoni