Ujumbe wa Leo kuhusiana na Furaha.
Posted by Unknown on 16:41 with No comments
Je wakati huu uliopo sasa na unaposoma mada hii, Je una furaha? Kumbuka kuna ambaye ana furaha wakati huu huu na ana kidogo ambacho hata na wewe hauna. Unafikiri ni nini kinachokukosesha furaha wewe ambapo mwenzako ana furaha kwa sasa wakati wewe hauna?
Furaha haipatikani kwa mali, sifa, umaarufu, utajiri wala cheo. Ingekuwa ni hivyo basi wenye pesa wangekuwa na furaha kuliko wenye shida na asingetokea mwenye shida akiwa na furaha kuliko mwenye mali hata kwa dakika chache. Kuna msemo unasema kuwa "Kuridhika ni utajiri mkubwa". Anayeridhika na kuwa na furaha kata kwa kidogo alicho nacho ana utajiri mkubwa kuliko mwenye kila kitu lakini bado haridhiki.
Badala ya kupoteza muda kuwaza matatizo uliyo nayo ambapo itakukoseshea furaha, waza bahati na baraka uliyonayo ambayo itakupa furaha. Furaha haipatikani nje yako kutokana na vitu na hali bali inapatikana ndani mwako. Ni wewe ndiye mwenye maamuzi.
FURAHA INAANZA KUPATIKANA NDANI YA NAFSI YAKO.
0 maoni:
Chapisha Maoni