Mambo Matatu ya Kukumbuka Unapokuwa Katika Wakati Mgumu Na Malengo Yako au Ndoto Zako.
Posted by Unknown on 13:00 with No comments
"Wakati mwingine fahamu kuwa kukosa unachokitaka ni bahati".
Shikilia Malengo Yako |
Wengi wanaishi na malengo yao akilini, kila mtu anaweza akawa na malengo yake. Sio kila mtu ana malengo lakini kuna ambao wana malengo tayari ya baadaye. Mfano Ndoto zako na Malengo yako kuhusu wakati ujao, maisha utakayoyaishi, watu unaopenda kushirikiana nao, mazingira ya baadaye, kazi yako itakayokuwa ya muhimu, kipato unachokadiria, familia itakavyokuwa au pia mbali na kuweka malengo ya mbali unaweza ukawa na malengo ya karibuni mfano kufaulu somo fulani, kupona ugonjwa fulani, au kutimiza lengo fulani kwa nia ya kusonga mbele zaidi kimaisha.
Lakini japokuwa unakuwa na malengo kuna hali zinazoweza kupelekea kuona malengo yako yanaenda taratibu, au malengo yako unaona hayatimii kwa wakati unaoutaka.
Pale unapoona umefikia hali ambayo akili yako inajikuta inachukuliwa na upepo wa mawazo hasi (negative thoughts and emotions) kama vile hofu, kukata tamaa, masikitiko, majuto, lawama, hasira na kadhalika ni hatari. Kuna wakati unakata tamaa kabisa. Hiyo hali hutokea na huweza kuwepo katika maisha na katika kujitahidi katika shughuli zako za maendeleo.
Kuna mambo mbalimbali ya kuweza kuyaweka akilini hasa pale unapokuwa katika kipindi ambacho ndoto zako zinaandamwa na giza au hali amayo inakukatisha tamaa.
1. Chunguza kilichopo akilini mwako.
Wakati huu unaweza ukawa na mawazo mbalimbali, fikra mbali mbali, ufahamu mbalimbali na vingi kuendelea katika akili yako. Vyote hivi vinaendelea katika akili yako. Unapokuwa katika hali hii unapaswa kuangalia akili yako inawaza nini kwa sasa. Kama unaona mawazo na fikra au hisia duni zinajitokeza basi ni vyema kuziondoa kwa kupanda hisia sahihi au mawazo sahihi. Mfano kama unaona kinachoendelea akilini mwako ni hofu basi badala ya kuipa hofu nafasi yape matumaini na uvumilivu nafasi. Chunguza unahofia nini, na kwanini? Kisha ondoa hofu. Hofu ni hisia na fikra ambayo haina uwezo wa kukusaidia kufika mahali bali inakuharibia uwepo wa matumaini. Vingine ambavyo unapaswa kuviondoa akilini ni lawama, kukata tamaa, mabaya, chuki, na vyote ambavyo unahisi vinakurudisha nyuma.
2. Tambua kinachokukwamisha.
Unapoona malengo yako na ndoto zako zinashindwa kufika pale unapotegemea basi tambua kuwa unaweza kubadili hali hiyo mfano kwa kuchambua sababu maalum ambazo zinakukwamisha na kisha tambua njia za kurekebisha hayo. Mfano kama una tabia au mazoea ambayo yanakurudisha nyuma ni sahihi kuyatambua na kuyarekebisha. Mfano unapenda kuwa na pesa za kutosha kutimiza mahitaji yako na una tabia na mazoea ya kutumia pesa vibaya, unatumia pesa kunywa pombe au unatumia pesa kwa ambayo hayana umuhimu unaweza ukaichunguza tabia hii na kujibadili. Badala ya kutumia pesa katika matumizi mabaya basi unakwenda kuitumia katika malengo sahihi na kuhifadhi kwa ajili ya akiba. Ni vyema kurekebisha kikwazo kinachokuzuia kutimiza mipango yako. Kama ukiona hakuna unachoweza kubadili au kikwazo kipo nje yako tafuta namna nyingine. Lazima utaiona njia tu.
3. Wakati mwingine kukosa unachokitaka ni bahati.
Unaweza ukawa na malengo fulani lakini usiyapate na ukaanza kusikitika na kuona kuwa unakosa amani. Kwanini unakosa amani? Je kama ungekipata unachokitaka na kingetokea kingine ambacho ni tatizo ungefanyaje? Mfano unapenda gari la aina fulani lakini kumbe ungelipata kuna tatizo lingetokea (ajali) lakini kwa kuwa hujalipata na tatizo hilo halijatokea huwezi kuona hilo. Ninachomaanisha sio usikitike tu kwa kila unachokikosa lakini kinachomaanisha hapa ni kujifunza kuwaza sahihi. Sio kwa upande mmoja tu. Tatizo likitokea tazama katika pande zote na kisha rekebisha. Hivyo ni bora kuliko kuumia kwa mawazo na fikra za upande mmoja.
Hakuna mwisho wa kuweka malengo ungali upo hai. Hata siku moja inatosha kupanga malengo yako upya na kuyatafuta. Usikate tamaa katika malengo yako, weka malengo yako akilini na kisha weka jitihada zako katika malengo yako na ipo siku utaweza kufikia pale unapotegemea.
0 maoni:
Chapisha Maoni