UPENDO - Njia Sahihi ya Kujitambua Na Kuishi Vyema.
Posted by Unknown on 13:48 with 1 comment
Ishi kwa Upendo, Upendo wa Kujijali, Kujali wanadamu Wengine, Kuheshimu kila kiumbe hai na kila kisicho Hai. |
Kutokwepo kwa upendo kunachangia maovu mengi na kupelekea watu kwenda njia ambazo sio sahihi. Upendo ni kinga na dawa ya matatizo mengi yanayomsumbua mwanadamu. Bila upendo huwezi kuwa salama kwani utaishi kwa wasiwasi wa kudhurika kwani hakuna anayekupenda.
Walimu wa kale wamefundisha kuwa UPENDO ni suluhisho la maovu mengi. Ki ukweli ukiwa una UPENDO hautaweza kumkosea mwanadamu mwenzako, na vitendo kama vile Chuki, Hasira, Tamaa na Ubinafsi huondoka kwani badala ya mtu kujijali yeye mwenyewe kwa mapenzi ya UBINAFSI basi hataweza kuishi na wengine.
Fikiria UPENDO ulivyo na nguvu. Upendo huunganisha roho na nafsi za watu. Upendo ni gundi inayoziunganisha nafsi zetu.
Nafsi zetu hutambua Upendo, na kwa kupitia Upendo nafsi zitu zinakua na Kujitambua zaidi |
Upendo sio tu uliozoeleka wa Jinsia mbili tofauti, upendo tunaouzungumzia hapa ni Universal Love, Upendo juu ya Ulimwengu na vyote vilivyopo, Upendo kwa wanadamu wengine bila kujali umri, jinsia, kabila, nchi, au imani/dini. Upendo juu ya mazingira, mimea, mito, milima na kila kitu. Ukiweza kuishi kwa kutazama upendo mkuu kama wa yule Aliyepelekea uwepo wa vyote hivi utaweza kuona maisha ni furaha na upendo huchochea furaha.
Ki ukweli ukiwa na upendo kwako wewe binafsi, upendo kwa wanadamu wengine na upendo wa kwa kila kinachokuzunguka utaishi kwa haki, na amani kabisa. Hutaweza kujidhuru wala hutaweza kumdhuru mwenzako kabisa.
Sio tu upende anayekupenda bali penda wote, kwa asiyeonyesha upendo kwako naye mpende. Sio umpende kwa malengo binafsi bali kutoka moyoni na itakusaidia daima. Penda bila kujali utapendwa au utalipwa bali penda na jizoeshe kupenda na kujali wanadamu wenzako.
Upendo ndio lugha pekee ambayo kila kiumbe kinauelewa... miti,wanyama(Kila chenye uhai) huelewa pale kinapopendwa.
JibuFuta