Ifahamu Tamaa ni Nini.

Posted by Apolinary Macha on 16:17 with No comments


Ni kutokana na tamaa fulani ndipo tendo fulani hufanyika, na kutokana na kufanyika kwa tendo fulani na matokeo fulani hufuata. Tunapozungumzia tamaa ni kama hali ya uhitaji wa kitu fulani au hali fulani ambayo unaamini baada ya kuipata hali au kitu fulani basi utapata furaha.

Tamaa huunganika na milango yetu ya fahamu. Kuna tamaa itokanayo na vitu vya kuonekana, ladha nzuri, harufu nzuri, sauti au tones nzuri, mguso n.k na vyote hivi tunategemea milango yetu ya ufahamu kuviexperience au kuvihisi.

Tamaa ikitekelezwa mara kwa mara hujenga mazoea. Na mazoea hayo tukiyakosa tunahisi kukosa furaha. Lakini tunasahau kuwa TAMAA HAITIMIZWI KWA KUTUMIA MILANGO YA FAHAMU BALI HUTIMIZWA MOYONI. Tamaa inaweza kukufunga na kupelekea kutamani kutimiza tamaa uliyonayo badala ya kuelewa kuwa tamaa haikamiliki. Hakuna mwanadamu asiye na tamaa ya aina yoyote, na pia tamaa inakamilishwa moyoni tu.

Tunasema kuwa tamaa ili ikamilike lazima toka moyoni mtu aridhike na tamaa hiyo huondoka. Lakini ukitaka kuitimiza tamaa nje yako (kwa matendo na milango ya ufahamu) utaikamilisha lakini utaendelea kuwa na tamaa nyingine kwani tamaa moja inaweza kujenga mazoea na mazoea hayo ukawa hauna furaha mpaka utimize tamaa fulani inayokuandama. Hivyo kuitimiza tamaa inayokuandanama ni sharti uikubali, na ufahamu kuwa kwa kutumia milango yetu ya ufahamu hatuwezi kuitimiza furaha ya tamaa bali ndio tunazidi kujiwekea mizizi ya kuwa wafungwa na tamaa hiyo.

Mfano siku chache zilizopita au muda fulani uliopita ulikuwa katika sherehe fulani na ulienjoy sherehe hiyo saaana. Lakini leo hii hauna tena ile furaha. Iliisha baada ya sherehe kuisha. Baada ya siku kuzidi kwenda nayo umeisahau na sasa unategemea furaha kuwepo kivingine.

Mfano una mazoea ya kuvuta sigara. Ukizoea utaona kuvuta sigara kunakupa furaha fulani lakini ukiimaliza kuivuta sigara hiyo na baada ya muda inakubidi kuivuta nyingine maana furaha unayoitaka haidumu.

Hivyo tamaa kamwe haina mpaka. Utatamani kitu fulani au hali fulani lakini baada ya muda utatamani hali nyingine au kitu kingine.

Tatizo sio kwamba tamaa ni mbaya bali tunapaswa kujifunza kuwa hatuwezi kutimiza tamaa zetu milele, pia inatupasa tuwe makini na aina ya tamaa tulizonaso hasa tamaa za ubinafsi, chuki, hasira na mazoea mabaya yanayoharibu miili yetu, akili zetu na nafsi zetu.