Badili mawazo yako kubadili maisha yako. Hatua za kubadili mawazo na fikra.
Posted by Apolinary Macha on 11:13 with No comments
Mawazo na fikra za mwanadamu huumba maisha ya mwanadamu. Fikra ulizonazo juu ya maisha yako, mwili wako, mitazamamo yako ni muhimu sana kwani huweka uhalisia katika maisha yako. Pale unapoamini jambo fulani, kuna nguvu unaikaribisha katika imani yako ya moyoni. Ndio maana ni vyema kuwaza mawazo/fikra nzuri kwa husaidia kuwa na mawazo chanya ambayo yatakusaidia katika mitazamo na maisha yako kwa ujumla. Ni vyema kila siku asubuhi kuamka na kushukuru kwa kuamka salama, kuwa na mawazo na fikra nzuri na kutoruhusu mawazo mabaya kukutawala. Epuka mawazo ambayo ni adui kwa mwanadamu mfano tamaa mbaya, mazoea mabaya, ubinafsi, choyo, uadui, chuki n.k ambavyo hunyonya nguvu yako ya asili.
Kuna
hatua mbalimbali ambazo mwanadamu anaweza akachukua pale anapotaka kubadili
mawazo. Kubadili mawazo au fikra ni muhimu sana kwani kama unapenda kubadili
maisha yako kuwa katika njia mbayo unapenda maisha yako yawe ni vyema kwanza
kubadilisha mawazo yoyote ambayo unayo kwani jinsi ulivyo au jinsi maisha
yalivyo kwako sio kutokana na uwezo wa nje yako bali ni kutokana na fikra na
mawazo yako. Mfano kama unatamani kuwa na roho nzuri ni vyema kuanza kuhisi
uwepo wa roho nzuri ndani yako, halafu amini uwepo wa roho nzuri upo na unaweza
kuutumia. Badala ya kuwa na hasira au chuki unaamua kujikumbusha kila wakati
kuwa unapaswa kuwa na roho nzuri. Cha ajabu ni kuwa tabia au mawazo yoyote
huweza kubadilika, na hubadilika pale unapoamua kweli na kujitolea kufanya
mazoezi. Mfano huo huo katika kuwa na roho nzuri, unaweza kujitolea katika kila
siku unafanya jambo lolote la kujikumbusha wema ulio nao moyoni, mfano kusaidia
au kujitolea muda, kitu, ushauri au chochote kumsaidia mwanadamu mwenzio katika
shida aliyo nayo.
Hatua
zifuatazo ni muhimu katika kubadilisha fikra au mtazamo wowote ulio nao ambao
unapenda uubadilishe.
1. Jizoeshe kurudiarudia mawazo, matukio au fikra nzuri.
Kila
unaporudia rudia wazo kichwani unajizoesha kuliamini na unalipa wazo hilo
nafasi ndani ya maisha yako. Mfano kama unaamini kuwa huwezi kufanya kitu
fulani, na kila saa unajisemea huwezi kufanya kitu fulani, basi unakaribisha
uwepo wa jambo lile katika maisha yako. Hivyo epuka mawazo au mazoea ya
kujisemea "siwezi kitu hiki" bali weka fikra na rudia rudia
kujisemea unaweza. Taaratibu utaona imani juu ya jambo unalolirudia inaongezeka
na unaona ni kama kweli, hapo inamaanisha imani yako inafanya kazi.
2. Hesabu furaha uliyo nayo na sio shida.
Pale
unapopenda kubadili mawazo fulani, ni vyema kushukuru kwanza kwa ulichonacho.
Maisha ni maajabu, unaweza ukawa unateseka na changamoto fulani kwa sababu
unaikataa, na pale unapoikubali changamoto kama sehemu ya mafundisho ya maisha
unakaribisha uwepo wa hali nyingine na ile hali ambayo unaiona ni changamoto
inakuwa sio changamoto bali sehemu ya furaha ya maisha, furaha ya kujifunza
changamoto zozote. Unaposhukuru kila jambo unakaribisha safari nyingine ya
maisha.
3. Weka nia katika kubadilika.
Katika
safari ya kutaka kubadili maisha yako inaweza ikakwama kwa sababu nia ni ndogo.
Unapoweka nia katika kubadilika na kuwa na imani juu ya nia hiyo, unapelekea
kutokea kwa mabadiliko. Safari yoyote inahitaji nia na imani.
4. Kuwa kiongozi wa mawazo yako.
Kila
sekunde kuna wazo katika ubongo, ni jukumu letu kuchagua mawazo ya kuyapa
kipaumbele akilini na kutoruhusu mawazo ambayo sio mazuri. Sisemi kwamba
unaweza kuamua ufikirie nini, bali mwanadamu kuwa na mawazo au thoughts
kichwani ni kawaida na huwa kila mwanadamu ana mawazo chanya na hasi. Mtu
mwenye busara huchagua mawazo chanya daima.
Kumbuka:
Wewe peke yako ndiye kiongozi wa safari yako ya maisha, na wewe ndiwe mwenye
maamuzi juu ya mawazo yako, fikra zako na maamuzi yako.
0 maoni:
Chapisha Maoni